skip to main |
skip to sidebar
MBUNGE WA TEMEKE ABBAS MTEMVU APATA CHAKULA CHA JIONI NA NA MARAFIKI ZAKE KUTOKA CHUO KIKUU CHA BUFFALO CHA NCHINI MAREKANI
Katika chakula cha jioni alichowaandalia marafiki zake katika maendeleo
kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo nchini Marehani, katika hoteli ya Sea
Cliff nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu
aliandaa cheki maalum ya urafiki kati ya Chuo hicho na Temeke.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) na Mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Buffalo cha Marekani, Tyler Choi wakati wa hafla ya chakula
cha usiki alichowaandalia marafiki zake hao jana kwenye Hoteli ya Sea
Cliff, Masaki Dar es Salaam.
Mtemvu (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya wageni kutoka Chuo Kikuu cha
Buffalo Marekani wakipata mlo wa usiku. Ujumbe huo umepangiwa kuonana na
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na
kutembelea baadhi ya shule na Hospitlai katika Jimbo la Temeke.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Ally (kushoto) na wenzie wakipata mlo huo
Mtemvu akidadiliana jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya African Maraika,
Fiona Barrelto (katikati) na mkewe Mariam wakati wa hafla hiyo.
Mfanyakazi wa Hoteli ya Sea Cliff (katikati) akichangamsha hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Sea Cliff wakiiimba wimbo huku wakipiga makofi ikiwa ni moja ya sham rashamra ya hafla hiyo.
Wageni ambao ni wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo Marekani wakiwa
wamesiamama walipokuwa wakitambulishwa kwenye hafla hiyo.
Mtemvu akielezea umuhimu wa ziara ya marafiki zake hao nchini.
Mwanafunzi Tyler Choi wa Chuo Kikuu ccha Bufalo akitoa shukurani kwa
kuandaliwa hafla hiyo pamoja na kuahidi kudumisha urafiki uliopo na
Mtemvu na Jimbo la Temeke kwa ujumla.
Barrelto ambaye ni mfadhili mkubwa katika sekta ya elimu Jimbo la
Temeke, akielezea umuhimu wa kudumisha urafiki uliopo kati ya chuo hicho
na Mtemvu (kushoto). Kulia ni Mke wa Mtemvu, Mariam ambaye pia ni
Diwani wa Viti Maalum Temeke.
No comments:
Post a Comment