ALIYEKUA KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA SASA MKOA WA TANGA NDUGU SALUM MOHAMMED CHIMA AAGA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA TAYARI KWENDA KURIPOTI TANGA
Katibu
Tawala mpya wa Mkoa wa Tanga aliyehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa Ndugu
Salum Mohammed Chima akizungumza katika hafla fupi ya kuagana na uongozi
wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia
Stella Manyanya (kulia) leo baada ya mabadiliko ya hivi karibuni ya Mhe.
Rais Jakaya Kikwete ambapo ameteua Makatibu Tawala wapya watano na
kuhamisha wengine akiwepo Ndugu Salum Chima. Katika salamu zake za kuaga
ameomba viongozi wote wa Mkoa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha
wanasimamia kikamilifu na kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa ya
Serikali na wahisani mbalimbali.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa salam zake za maagano
ambapo alisikitika kwa uhamisho wa kiongozi huyo ambaye kwake alikua
kiungo muhimu na msaada mkubwa katika mambo ya kiutendaji. Aidha
alisisitiza juu ya kuchapa kazi na ushirikiano baina ya viongozi wa Mkoa
na wananchi katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akitoa neno kwa niaba ya
Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Rukwa, alisema kuwa kwa Ndugu Chima
kuhamishiwa Mkoa wa Tanga ambao ni Jiji akitokea Mkoa mdogo wa Rukwa ni
"promotion" na anastahiki pongezi kwani uwezo wake wa kuchapa kazi ndo
umemfikisha hapo alipo. Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa sifa kubwa ya
Ndugu Chima ni uwezo wake mkubwa wa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka
kwa wakati sifa ambayo ni muhimu kwa viongozi wa sasa katika maendeleo
ya taifa letu.
Katibu
Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Ndugu Samson Mashalla
(kulia) akiongea kwa niaba ya watumishi wote wa Sekretarieti ya Mkoa wa
Rukwa. Alieleza kushtushwa na uhamisho huo uliokuwa wa ghafla ambapo kwa
watumishi umekuwa ni kusikitisha kutokana na ukaribu, upole na upendo
aliokuwa nao Ndugu Chima. Ndugu Chima aliwapenda watumishi wote wa ngazi
za juu hadi za chini bila ubaguzi wa aina yeyote.
Baadhi
ya viongozi na watumishi walihudhuria katika hafla hiyo fupi ya
maagano. WATUMISHI WOTE NA VIONGOZI WA SERIKALI YA MKOA WA RUKWA
WANAMTAKIA NDUGU CHIMA KILA LA HERI KATIKA KITUO CHAKE KIPYA CHA KAZI
AMBACHO NI MKOA WA TANGA. Tunaamini kuwa Tanga imepata kiongozi thabiti
mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza katika kutoa maamuzi sahihi na ya haraka
kwa muda muafaka, "tunaomba apewe ushirikiano atafanya". Kwa upande
wake Katibu Tawala Mteule wa Mkoa wa Rukwa kwa sasa ndugu Symthies
E.Pangisa aliyekuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara anakaribishwa
kwa dhati Mkoani Rukwa na ameahidiwa ushirikiano katika kusukuma
gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. Picha na Habari na Hamza Temba -
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment