Monday, 20 January 2014

AJALI YAUWA 13 MKOANI SINGIDA

 Taarifa inasema gari aina ya NOAH ilikuwa imebeba abiria kutoka Itigi wakielekea Singida Mjini. Dereva na utingo wa Lori walikimbia baada ya ajali hiyo kutokea.
  Imetokea ajali mbaya huko Singida ambapo gari aina ya NOAH na Lori la mizigo yamegongana uso kwa uso na kisha gari hiyo aina ya NOAH kuingia chini ya uvungu wa Lori na kusababisha vifo vya watu hao 13 ambao wote walifia katika eneo la ajali.
CHANZO: ITV BREAKING NEWS.
 
WAKATI HUOHUO AJALI NYINGINE KARATU.....

Watu sita wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na machimbo ya moram hapa wilayani Karatu.

Machimbo hayo yako karibu na shule ya Sekondari Mlimani. Hali ni tete ni majonzi kila kona.

Habari zaidi zinasema kuwa huenda kuna watu zaidi ndani ya machimbo hayo na mkurugenzi wa Halmashauri ameagiza grader kwaajili ya kuendelea kufukua zaidi.

HABARI NA PICHA TUTAWALETEA HIVI PUNDE....STAY TUNNED!!!!

R.I.P. Vijana 6 wa kitanzania waliofariki katika kutafuta riziki.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!