Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akisisitiza
jambo wakati akiwatangaza washindi wa droo ya wiki ya tisa ya promosheni
ya Airtel Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa jana na kuwapata washindi wa
pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 na kumpata Edwin Edmund
Kajimbo kutoka Iringa aliyejishindia tiketi mbili ya safari
iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya
Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford. Kushoto ni
Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akimpigia simu
Bw. Edwin Edmund Kajimbo mkazi wa Iringa aliejishindia tiketi mbili ya
safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya
Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford, katika
droo ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa. Wakati wa droo hiyo
iliyochezeshwa jana, washindi 14 wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi
milioni 22 walipatikana. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya
kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imeendelea kuwapa faraja washindi
wake wa promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ kwa kuwazawadia zaidi ya pesa
taslim shilingi milioni 194 na kutoa tiketi 18 za safari iliyogharamiwa
kila kitu ya kwenda Old Trafford nchini Uingereza.
Kampuni
hiyo ya mawasiliano jana imetoa shilingi milioni 22 pesa taslim kwa
washindi 14 na tiketi mbili za kwenda Old Trafford kuangalia mechi ya
ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’, kwa mshindi mmoja wa kila
wiki katika wiki ya tisa ya promosheni ya Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa
katika ofizi ya makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya droo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando
alisema promosheni ya Mimi ni Bingwa imekuwa ikiwapa faraja watanzania
wengi ambao wamekuwa wakionyesha furaha zao za ushindi wa pesa taslim au
safari inayogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford.
“Tumekuwa
tukipokea maoni kutoka kwa washindi wetu, hususani wale waliojishindia
pesa taslim, wakisema pesa waliojishindia toka promosheni ya Mimi ni
Bingwa wameipata wakati muafaka wakihitaji zaidi msaada wa kifedha.
“Wanasema
miezi iliyochaguliwa kwa ajili ya promosheni na pesa walizopokea bila
jasho kutoka Mimi ni Bingwa promosheni, zimeweza kuwaongezea uwezo wa
kifedha ili kupambana na hali ngumu ya kiuchumi katika miezi hii migumu
inayohitaji fedha nyingi. Tumekuwa tukituma milioni moja (1m/-) kwa
washindi wetu mara tu baada ya kuwatangaza kupitia Airtel money na
kuweka shilingi milioni tano (5m/-) katika akaunti za washindi baada ya
kupata taarifa zao za benki,” alisema Mmbando.
Aliongeza
kuwa promosheni hiyo ya Mimi ni Bingwa iliyoanza mwishoni mwa mwezi wa
Novemba mwaka jana, imelenga kurudisha sehemu ya pato la kampuni kwa
jamii inayoizunguka na kuwaunganisha mashabiki wa soka na michezo ya
kimataifa.
Alimtangaza
Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa kuwa ni mshindi wa wiki hii wa
tiketi mbili wa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia
mechi za klabu ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.
Bw.
Kajimbo anakuwa ni mshindi wa tisa wa tiketi toka promosheni ilipoanza
baada ya Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam,
Bw. Shaibu Rashid Dege, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nang’olo katika wilaya
ya Kilwa - Mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph
Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob
kutoka Njiro mkoani Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani
Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na
Salma Juma Mughery kutoka Dar es Salaam, waliojishindia tiketi katika
droo za kila wiki zilizopita.
Mmbando
pia aliwatangaza washindi wawili wa shilingi milioni 5 kila mmoja wa
wiki kuwa ni Bw. Uruma Samwel Mkongwa kutoka Usa River mkoani Arusha na
Filemon Nathaniel Mgaya kutoka Dar es Salaam pamoja na washindi wengine
10 waliojishindia shilingi milioni 1 kila mmoja.
“Zaidi
ya shilingi milioni 324 zilitengwa kama zawadi ya pesa taslim kwa ajili
ya promosheni ya Airtel ya Mimi ni Bingwa, inayowapa fursa washiriki wa
Mimi ni Bingwa kushinda kila siku na kila wiki,” alisema.
Mmbando alisema kuwa mwenendo wa washiriki wa Mimi ni Bingwa kuendelea kujikusanyia pointi unazidi kutoa amasa.
“Bado
kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa, ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa
ya shilingi milioni 50. Nawaasa wateja wa Airtel ambao bado
hawajajisajili katika promosheni hii kuwa hawajachelewa; bado kuna
zawadi nyingi zaidi kushindaniwa. Ili kuingia katika promosheni hii
mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BNGWA” kwenda
namba 15656, kwa kujibu maswali mengi iwezekanavyo, unaweza kuwa mshindi
wa milioni 50 au zawadi nyinginezo nyingi,” alisema.
No comments:
Post a Comment