Sunday 26 January 2014

ABIRIA 17 WANUSURIKA KUFA BAADA YA NDEGE KUFELI BREKI ILIPOKUWA IKITUA

 Abiria 17 akiwemo waziri wa katiba na sheria Zanzibar Mhe. Abubakari khamis bakar, na marubani wawili, wamesalimika kifo baada ya ndege ya shirika la ndege la ‘Zanz air’ kufeli breki, muda mfupi wakati ndege hio ilipo kuwa ikitua  kwenye uwanja wa ndege wa Abeid amani karume, uliopo nje kidogo ya mji wa chakechake mkoa wa kusini Pemba.

Kwamujibu wa tarifa zilizo tolewa na makamanda wa polisi mkoa kusini Pemba  kamishina msaidizi  swalehe mohamed swalehe na kamanda wa kikosi cha zima moto na uokozi pemba wamesema ndege hiyo wakati wa kutua ilipata ikhitilafu ya kufeli breki na kusereka hadi nje ya uwanja  umbali wa mita miambili kwenye vichaka
 Wamesema abiria wote wametoka salama hakuna alie juruhiwa    licha ya ndege hio kuacha uwanja kusereka kwenye nyasi na kungia kwenye mashamba ya muhogo kupita kwenye masiki majiti yalio katwa nakisha kusimama baada ya ringi kujizonga namizizi ya pori hilo.
 Ipo haja kwa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini kutoa taluma kwa watendaji wa kiwanja cha ndege kisiwani pemba kutoa ushirikiano kwa wandishi wa habari pale inapo tokea dharura kutokana na watendaji wa kiwanja chandege kisiwani hapa kushindwa kabisa kutoa usjhirikiano kwa wandishi juu ya tukio hili

CREDIT. IPP MEDIA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!