skip to main |
skip to sidebar
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, DKT. EMMANUEL NCHIMBI AZINDUA RASMI KIWANDA CHA USHONAJI CHA GEREZA KUU BUTIMBA, MWANZA PAMOJA NA MAGEREZA “DUTY FREE SHOP” YA KANDA YA ZIWA LEO JIJINI MWANZA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi( suti nyeusi) akiangalia nguo za aina mbalimbali kama ambavyo zinaoonekana katika picha ambazo zimeshonwa na Wafungwa katika Kiwanda cha Gereza Kuu Butimba, Mwanza ambapo Kiwanda hicho kimezinduliwa rasmi leo Disemba 02, 2013(kushoto kwa Dkt. Nchimbi) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja. M
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(Mb) akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa Magereza “Duty Free Shop” iliyopo Gereza Kuu Butimba, Mwanza ambayo itahudumia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa leo Disemba 02, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Butimba( kulia) ni Rais wa Transit Military Shop Limited, Bw. Sadrudin Virji( nyuma kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
No comments:
Post a Comment