
Waziri Mkuu mstaafu katika Serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye, amesema wapinzani wake kisiasa ‘wanampakazia’ kuwa ni masikini wa kutupwa, hivyo kukosa uwezo wa kuwapa fedha wanaomuunga mkono.
Alisema kauli hiyo inatolewa na wanasiasa wanaopinga jitihada zake za kupinga rushwa, ufisadi na aina nyingine za uovu kwa jamii ya Watanzania.
Sumaye, aliyasema hayo jana, alipokuwa akizungumza kwenye harambee ya kuchangia shughuli za ujenzi katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mawella iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro na hotuba yake kupatikana kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.
Alitoa mfano akisema, “kuna kiongozi mwanasiasa (hakumtaja jina) aliwakuta watu wanaoniunga mkono wakinijadili, akawaambia huyo Sumaye ni maskini atawapa nini? Jiungeni na kambi ya fulani atawapeni fedha nyingi na shida zenu zitaisha.”
Kwa mujibu wa Sumaye, mwanasiasa kiongozi huyo alisema umasikini si sifa ya kuwa Rais wa nchi.
Alielezea kusikitishwa na kauli hiyo kwa vile hajawahi kutangaza azma ya kuwania urais wa Tanzania.
“Pili, mimi sio masikini ila ni kweli sina fedha za kuwanunua wapiga kura wala utaratibu wa kuwanunua siutaki, kwa maana ni rushwa,” alisema.
Alisema si sahihi kuitwa masikini kwa sababu alikuwa Naibu Waziri na Waziri kamili kwa karibu miaka tisa, na hatimaye Waziri Mkuu kwa miaka 10 bila kufukuzwa kazi, hivyo hayumo katika kundi la masikini
No comments:
Post a Comment