
Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa sana na wananchi mwaka huu ni kitendo cha Bunge kupitisha uanzishwaji wa tozo ya kodi ya TShs. 1,000/- kwa kila laini ya simu. Hii ilikuwa wakati wa Bunge la Bajeti la mwaka 2013/2014.
Kufuatia hali iliyojitokeza, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kutoa agizo kwa wahusika kulishughulikia suala hilo.
Taarifa kutoka Ofisi ya Rais zimethibitisha kuwa wahusika walilifanyia kazi suala hilo na kuliwakilisha kwa Rais. Na leo Mheshimiwa Rais ametia sahihi Hati ya Dharura (Certificate of Emergency) kufanyika marekebisho kwa Muswada wa Fedha wa mwaka 2013 kuondoa tozo ya kodi kwa laini za simu (SimCard Tax).













No comments:
Post a Comment