Friday 27 December 2013

MWANADADA JACKIE CLIFF(VIDEO QUEEN) ADAIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA

Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

Kwa mujibu wa mtandao wa China Daily ambao hata hivyo haukujata jina la mrembo huyo,  mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.

Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013.


Licha ya habari kushindwa kubainisha  mwanamke huyo ni nani, baadhi ya wachunguzi wa mambo toka kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii waliweza kubaini kuwa inawezekana mwanadada huyo akawa  ni Jackie Cliff kutokana na sababu zao binafsi wanaouzijua wao na pia ikizingiatiwa kuwa mwanadada huyo alikuwa nchini China kwa muda mrefu akizunguka kwenye mitaa na majimbo mbalimbali ya nchi hiyo yaliyotajwa kwenye habari hiyo.

JAMANI, huyu dada aliyekamatwa awe Jackie Cliff au mdada mwingine asiyefahamika au hata kama sio mtanzania la muhimu hapa siyo kukamatwa kwake, bali ni sisi kama vijana tunaotafuta maisha kutokupenda shortcut hizi za mafanikio.
Sisi kama bongomovies tunaamini mtu yoyote unaweza kufanikiwa vizuri kabisa hata kama hujasoma tena kwa njia za halali kabisa ambazo hazihatairishi maisha yako wala ya watu wengine.
Kubeba dawa za kulevya sio suluhu ya maisha na kupata hela. Siku zote kumbuka hamna marefu yasiyo nan cha, na ipo siku utakamtwa na waliokutuma watakusahau au utaishia kunyongwa tu! tusikimbie shule, na kama tushakimbia tutumie vipaji kama uigizaji, muziki, na michezo kupata mafanikio kimaisha. Tazama watu kama Marehemu kanumba, Diamond au hata Juma kaseja. UKIAMUA INAWEZEKANA! Tubadilike jamani.
NA BONGO MOVIE.....

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!