Thursday 26 December 2013

MAMA MJAZITO AJIFUNGUA KWENYE KORIDO BAADA YA KUFUKUZWA WODINI


 Kulia ni Rhoda Mwakyusa(50), akifuatiwa na mwanaye Sabina Mwakyusa
 Mwafyela(28), mume wa Sabina na Dada yake Sabina kushoto.


 Sabina Mwakyusa(28) anayedai alifukuzwa na manesi wodini na kujifungulia nje
 ya geti usiku huku mvua ikinyesha akiwa na Mama yake mzazi, Rhoda Mwakyusa(50).

 Mtoto aliyezaliwa usiku nje ya geti la Hospitali ya Ifisi Mbalizi, baada ya mama
 yake kudaiwa kufukuzwa akiwa na uchungu.


*Walinzi wamsaidia.

Na Gordon Kalulunga, Mbeya

HOSPITALI teule ya wilaya ya Mbeya(Ifisi-Mbalizi), imekumbwa na
 kashfa ya kufukuza wajawazito wodini kisha wajawazito hao kujifungulia
 katika mazingira yasiyo na staha nje ya hospitali.



Tukio la hivi karibuni limetokea usiku wa Desemba 19, mwaka huu, ambapo
 baadhi ya wauguzi waliokuwepo katika chumba cha matazamio ya kujifungua,
 wanadaiwa kumfukuza na kumpiga mjamzito Sabina Mwakyusa(28) mkazi
 wa Kijiji cha Iwala, kata ya Utengule Usongwe wilayani humo.



Akizungumza na kalulunga media blog, Sabina, alisema alifika hospitalini
 hapo Desemba 18, mwaka huu na alipimwa na manesi ambapo walimwambia
 kuwa hawamuoni mtoto tumboni mwake.



‘’Baadaye akaja Daktari na kunipima, akaniambia mtoto anaonekana vizuri
 na ningejifungua mtoto wa kike ndipo nikaendelea kusubiri uchungu zaidi’
’ alisema Sabina.



Alisema ulipofika usiku wa Desemba 19 majira ya saa mbili usiku, alianza
 kujisikia uchungu, ndipo manesi waliompima mwanzo wakamwambia

 anatakiwa apimwe tena jambo ambalo alikataa kwa madai kuwa alikuwa
 akiumizwa, ndipo wakamwambia aondoke hospitalini hapo kwasababu ana
 kiburi.



‘’Baada ya kuonekana mimi nasita kuondoka, wakaanza kunipiga na kunipatia
 biki na kunilazimisha kuandika kuwa mimi sitaki kujifungulia hapo ndipo
 tukatoka na mama na kwenda nje ya geti na kujifungulia getini huku mvua
 ikinyesha’’alisema Sabina Mwakyusa.



Alisema, mama yake na baadhi ya wajawazito waliokuwepo ndani ya wodi
 hilo, walijaribu kuwabembeleza wasimfukuze lakini walikataa.



Mama mzazi wa mwanamke huyo, Roda Mwakyusa(50), alisema anaumia
 akikumbuka yaliyomkuta mwanaye ikiwa ni uzao wake wa kwanza.



‘’Niligaragara mweeeh! kuwaomba msamaha wale manesi ili wamsamehe
 na kumhurumia huyu mtoto wangu, lakini walikataa wakisema kuwa ana kiburi
 sana’’ alisema Prisca Mwakyusa.



Alisema walipotoka wodini huku mwanaye uchungu ukimzidi, walifika getini
 akazidiwa. Chupa ikapasuka. Damu zikaanza kumvuja; alikaa muda mrefu
 zaidi ya saa moja na kuanza kujifungua ndipo walinzi wa kampuni ya Mult-Lion,
 wakamsaidia kumpeleka katika upenu wa duka la hospitali hiyo ili kukwepa
 kokoto zilizopo na mvua iliyokuwa ikinyesha.



Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Mult-Lion, Kinanda Sanga, alipoulizwa
 kuhusu tukio hilo, alisema kuwa hakuwa na taarifa lakini baada ya kuwauliza 
askari wake walimpatia taarifa ya tukio hilo kuwa lilitokea na wao wakatoa
 msaada.



Dada wa msichana huyo, Enitha Mwakyusa(35), alisema alipigiwa simu

 majira ya saa tano usiku na mama yake mzazi akimweleza yaliyomkuta mdogo
 wake na kwamba atafute gari la kwenda kuwachukua.



‘’Mama alinipigia simu usiku, nikawaamusha majirani ambao walikuwa
 na namba za madereva tax, ambapo saa saba walifika hapa nyumbani
 Mapelele’’ alisema Enitha.



Wifi wa Sabina Mwakyusa, Prisca Nafred, alisema alimpeleka mtoto
 aliyezaliwa katika hospitali hiyo majira ya saa saba mchana ya
 Desemba 20, kwa ajili ya chanjo, lakini hakupata chanjo kwa madai
 kuwa alikuwa amechelewa kufika, hivyo alitakiwa kufika siku ya Jumanne
 Desemba 24, mwaka huu.



Desemba 21, familia hiyo ilimpigia simu Mwandishi wa habari wakimweleza
 kuhusu maendeleo mabaya ya mtoto ambapo Mwandishi wa habari hizi 
alimtaarifu Mratibu wa afya ya mama na mtoto mkoa wa Mbeya, 
Prisca Butuyuyu, kuhusu suala hilo ambapo makubaliano yaliafikiwa
 kuwa mtoto apelekwe Hospitali ya Rufaa, kitengo cha wazazi Meta.



Mtoto huyo alipokelewa Meta na kuingizwa kwenye chumba cha joto kisha 
kuanza kupatiwa matibabu kwa kuwekewa drip za maji mpaka Desemba 23 
mwaka huu.



Mganga Mkuu wa wilaya ya Mbeya Louis Chomboko, alipopata taarifa,
 alichukua hatua ya kwenda kumuona mtoto huyo katika hospitali ya Meta.



‘’Nimeonana na mama wa mtoto na kumuona mtoto chumba cha joto na kupata maelezo yote ikiwa ni pamoja na maelezo ya file la Meta hivyo nipe nafasi tena kufuatilia tukio hili hospitali ya Ifisi na tukibaini ukweli tutachukua hatua’’ alisema Dr, Chomboko akimsihi Mwandishi kutoandika kwanza habari hii.



Mganga mkuu wa hospitali ya Ifisi Mbalizi, Msafiri Kimaro, Desemba 23, 

mwaka huu, alipotakiwa kuzungumza na mwandishi wa habari, aliitisha kikao
 cha wauguzi wanne waliokuwepo siku ya tukio, Muuguzi mkuu, muuguzi
 kitengo cha chanjo idara ya Mama na mtoto na katibu wa hospitali hiyo.



Alisema katika hospitali hiyo, wanawake zaidi ya 300 wanajifungulia hapo
 lakini tukio kama hilo hakumbuki kuwahi kujitokeza ingawa Muuguzi mkuu 
alikiri kuwa anayeonekana kukataa kupata huduma hapo anaandika maelezo
 na kuruhusiwa kuondoka.



Dr. Kimaro, aliwauliza wauguzi waliokuwepo siku ya tukio, ambapo walikubali
 kumfahamu mjamzito huyo na kukubali kuwa alikuwa chini yao na kwamba
 alikataa kupata huduma hospitalini hapo na kuamua kuondoka.



‘’Ilipofika saa mbili alipatwa uchungu na tulipotaka kumpima kwa kumwingiza 
vidole sehemu za siri alikataa na pia siku ya kwanza alitusumbua sana na kubana
 miguu, ndipo akaandika maelezo mafupi kuwa hakutaka kupimwa bali kwenda
 yumbani kwake’’ alisema Tumaini Mgimwa.



Aliongeza kuwa mama yake mzazi wa Sabina, alimbembeleza mwanaye ili
 akubali lakini alikataa ndipo mama yake akaanza kulia akimtaka akubali
 lakini hakuweza kukubali kutibiwa hospitalini hapo.



‘’Muuguzi mkuu wa hospitali hiyo, Sikitu Mbilinyi, alisema yeye alikuwepo
 siku hiyo na alipoitwa akakutana na mgonjwa lakini mjamzito huyo alikataa
 kutibiwa ndipo akawaambia manesi kuwa mgonjwa asiondoke mpaka asaini
 kuwa hataki kutibiwa’’ alisema Mbilinyi.



Alisema mgonjwa kukataa au kukubali kupewa huduma na hospitali au daktari
 fulani ni haki yake lakini wengi hawajui haki zao na kwamba mjamzito huyo
 alipojifungulia katika geti la hospitali hiyo, mama yake angepaswa kuingia 
ndani ambako anadai eti wangempatia msaada.



Katibu wa hospitali hiyo, Goodluck Lession, alisema swali la msingi ni kwamba
 iweje mjamzito afike tangu Desemba 18 mpaka usiku wa kuamkia Desemba 20
, kisha aseme kuwa hataki kupata huduma hospitalini hapo?



Goodluck, alisema hayo baada ya swali kutoka kwa mwandishi kumhoji
 muuguzi mkuu Mbilinyi swali hilo.



Kwa upande wa kiongozi wa kitengo cha chanjo hospitalini hapo, alisema
 kuwa kukataliwa chanjo mtoto huyo ni kutokana na dawa ya chanjo inatakiwa
 chupa moja kuchanjwa watoto kumi.



‘’Tunafanya hivyo kwasababu endapo mtu ukichanja mtoto mmoja, inatakiwa
 dawa hiyo uiandikie maelezo hivyo tunaogopa’’ alisema kiongozi huyo.



Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya kanisa la Uinjilisti Tanzania, ambalo
 linamiliki hospitali hiyo na serikali kuingia ubia,  Tito Nduka, alipohojiwa
 kuhusiana na jambo hilo, alisema kuwa amepata taarifa kuwa hospitali
 imeshusha ufanisi wa kazi.



‘’Kwanza kamati kuu yetu imepata taarifa za kudhorota kwa huduma
 kwa ujumla, lakini Mganga mkuu ni mwadilifu na msikivu, katika jambo hilo
 tutakaa na viongozi na kulikemea’’ Alisema Nduka.



Katibu Mkuu wa maendeleo ya kanisa hilo, JaCkob Mwakasole, alisema taarifa
 za kushuka kwa ufanisi wa huduma katika hospitali hiyo wamezipata na kwamba
 tukio hilo haliwezi kupita hivi hivi.



Mratibu wa afya ya Mama na mtoto mkoa wa Mbeya, Prisca Butuyuyu, alisema
 kuwa….



Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya, ………. Seif Mhina, alisema kuwa…



Baadhi ya wauguzi na madaktari wa hospitali hiyo ambao hawakutaka majina 
yao kuandikwa, wamekiri kuwepo kwa udhorotaji wa huduma za afya katika
 hospitali hiyo tangu ubia wa serikali na kanisa  na kwamba mpaka sasa kuna
 maelewano hasi kati ya waajiriwa wa serikali na wale wa kanisa jambo ambalo
 wanaoumia ni wagonjwa.



Wakati hayo yakiedelea kutokea nchini, malengo ya milenia yanaeleza kutaka 
kupunguza vifo vya mama na mtoto ifikapo mwaka 2015.



Hayo yanabainika katika utafiti wa umoja wa Mataifa, unaongelea "ndoto" ya
 kufikia malengo nane ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) zaidi katika afya:
 kupunguza vifo vya watoto wachanga (Lengo la 4), kuboresha afya ya
 wajawazito (lengo la 5) na kukabiliana na VVU/UKIMWI, malaria na 
magonjwa mengine (Lengo 6).



Baadhi ya viongozi wa dunia wanaoongoza mtandao wa kutoa        
 msukumo wa kisiasa ni pamoja na Rais Michelle Bachelet wa Chile, 
 Rais wa Msumbiji Armando Guebuza na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.



Daktari bingwa nchini katika masula ya uzazi, Dr. Moke Mgoma, kutoka shirika
 la Evidence for action(E4A), alipohojiwa alisema alichotendewa
 Sabina Mwakyusa, ni kitendo kibaya ikizingatiwa kuwa serikali 
inafanya jitihada kuondoa ukatili wa baadhi ya wauguzi.



Mwezi Desemba mwaka 2012, Mama mmoja(jina tunalo), aliyekuwa 
anaumwa BP, alichomwa sindano (dawa)ambazo haziendani na ugonjwa

 wake na mmoja wa watoto wake alipohoji kwa uongozi wa hospitali hiyo
 alijibiwa kuwa hapaswi kugombana na wauguzi! Kisha akaitwa Dr. Kenneth, 
ambaye aliamua kuokoa maisha ya mama huyo katika hospitali hiyo ya Ifisi kwa 
kumchoma sindano ya dawa iliyokuwa ikitakiwa

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!