Tuesday, 31 December 2013

MADUKA YAFUNGWA MWANZA KUPINGA MASHINE ZA TRA





WAFANYABIASHARA jijini Mwanza jana walifunga maduka yao, kupinga kutumia mashine za kielektroniki (EFD) za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zinazotumika kutoa risiti wakati wa kuuza bidhaa zao.


Mgomo huo ulileta tafrani kati ya uongozi wa TRA jijini Mwanza na Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao kwa pamoja waliwaunga mkono wafanyabiashara kugomea mashine hizo.
Wafanyabiashara hao waliamua kutofungua maduka yao, wakipinga kulazimishwa kununua mashine wanazodai zinauzwa kwa bei kubwa kati ya Sh 600,000 na Sh 800,000.
Mbali na kufunga maduka yao, wafanyabiashara hao walikuwa wamepanga kuandamana kwenda katika ofisi za Mamlaka ya Mapato majira ya saa mbili asubuhi, lakini maandamano yao yalizuiwa na Polisi .
Ulinzi uliimarishwa jijini kuhakikisha hakuna mikusanyiko yoyote ya makundi ya watu.
Akizungumza ofisini kwake, Meneja TRA Mkoa wa Mwanza, Jeremiah Lusana alisema mashine hizo lazima zitumiwe na wafanyabiashara ili kuepuka taifa kupoteza muda na mapato

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!