Tuesday 24 December 2013

JK ATOA ZAWADI YA XMAS KW A WATOTO YATIMA NA WAZEE WASIOJIWEZA



Na Kiza Sungura-MAELEZO,Dar es salaam 
 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho kikwete ametoa jumla ya kilo za mchele 1,200 , lita 220 za mafuta na mbuzi 25 kwa ajili ya zawadi ya sikukuu ya Krismas kwa makundi maalum. Zawadi hizo zilikabidhiwa jana (leo) na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bibi Beatrice Fungamo kwa niaba ya Rais Kikwete kwenye sherehe fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es salaam. 



 Alisema kuwa Rais Kikwete ametoa zawadi ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum kama vile yatima, wazee wasiojiweza na watato walioko katika mkinzano na Sheria ili nao waweze kuungana na Watanzania wengine katika kusherekea sikukuu ya Krismas. Bibi Fungamo alisema kuwa nje ya kutoka zawadi kwa vituo mbalimbali vya Mkoa wa Dar es salaam pia ametoa katika makunndi mengine ya mikoa mingine hapa nchini. 
 Alisema kuwa kwa upande wa Dar es salaam ametao kwa vituo 11 vinavyosaidia kutoa huduma kwa watoto na wazee wasiojiweza ambazo ni Kituo cha Watoto Ibn Kathir, Tabata, Ilala, Makao ya Watoto Kurasini, Temeke, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Kituo cha Kwetu Mbagala Girls Home, Kituo cha Yatima Group, na Kituo cha CHAKUWAMA. Vingine vya mkoani Dar es salaam ni Mahabusu ya Watoto, Makao ya Watoto Yatima Mburahati, Kituo cha Tuwapende Watoto Bunju, Makao ya Wazee wasiojiweza Msimbazi na Vosa Mission Kongowe. 
 Alisema kuwa kwa vituo vya mikoani na maeneo mengine nje ya Dar es salaam zawadi zao watapatiwa katika maeneo yao . Bibi Fatuma alivitaja vituo vya nje ya Dar es salaam vilipatiwa zawadi na Rais Kikwete ni Kituo cha Mabaoni Chakeckale Pemba, Kituo cha Werezo cha Unguja, Mahabusu ya Wototo Moshi mkoani Kilimanjaro na Makao ya Wazee wasiojiweza Sukamaela mkoani Singida. Vingine ni Makao ya wasiojiweza Bukumbi, Misungwi mkoani Mwanza na Makazi ya Wazee wasiojiweza Msufini , Muheza mkoani Tanga. 
 Alisema kuwa Rais Kikwete ametoa zawadi hizo kwa kutambua kuwa watoto na wazee hao wanapaswa kujumuika na wanajamii wengine katika kusherehekea sikukuu hiyo vema. 
 Hatua hii ya Rais Kikwete ni sehemu ya utamaduni wake aliojijengea wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali .


 Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (katikati) akimkabidhi  Mwakilishi wa Makao ya Watoto Kurasini wilayani Temeke Bibi  Beatrice Mgumiro mbuzi watatu, kilo 150 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa ni zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu kwa furaha.

 Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Mkuu wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto Ramadhani Yahaya (kulia)  mbuzi wawili (2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu kwa furaha.
 Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Msimbazi  Sister Maria Silvana  (kulia)  mbuzi watatu, kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Mkurugenzi WA  Kituo cha Vosa  Mission Hochimin Mugarura (kulia)  mbuzi wawili, kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu.  Picha na MAELEZO, Dar es salaam

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!