Friday 27 December 2013

DOKTA AMSHAURI BANZA STONE KUPUMZIKA KUTOKANA NA AFYA YAKE




MSANII nguli wa muziki wa dansi, Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ ameshauriwa kupumzika kazi za nguvu ikiwemo uimbaji kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.


Akizungumza na paparazi wetu, daktari mmoja wa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar aliyeomba jina lake lisitajwe gazetini, aliyemshuhudia Banza siku za hivi karibuni akiimba jukwaani, alisema kwa hali aliyonayo msanii huyo hatakiwi kuutumikisha mwili wake.


Daktari huyo alisema kutokana na uzoefu wake wa kitabibu, mwili unapofika hatua ya kuugua mara kwa mara unahitaji tiba maalumu ikiwemo muda mwingi wa kupumzika.

Aidha, aliongeza kuwa endapo mhusika atashindwa kuzingatia maelekezo hayo, anaweza kukumbwa na matatizo makubwa zaidi na hatimaye kuweza kupoteza maisha.

Huyu Banza anatakiwa apumzike, afya aliyonayo kwa sasa haimruhusu kabisa kuutumikisha mwili wake kwa kazi nzito kama za jukwaani, vinginevyo atajisababishia matatizo makubwa ikwemo kufa kabla ya muda wake,” alisema dokta huyo.

Mwandishi wetu alimtafuta Banza Stone na kumgusia juu ya ushauri huo ambapo alikiri kuwa na afya isiyoimarika huku akiahidi kuuzingatia ushauri aliopewa.

Ni kweli afya yangu haijakaa sawa, lakini si unajua mambo ya kujitafutia riziki, ila nitaufuata na kuufanyia kazi ushauri wa daktari huyo,” alisema Banza Stone a.k.a Mwalimu wa walimu

GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!