Friday, 20 December 2013

BREAKING NEWS. WATU SABA WAFARIKI KUJERUHIW VIBAYA KWA AJALI YA BASI


Watu 7 wamekufa papo hapo na wengine wengi inasemekana wamejeruhiwa baada ya basi la Allys linalofanya safari zake kati ya DSM na Mwanza kugongana uso kwa uso na Hiace katika eneo la Buhongwa mkoani Mwanza.

WAKATI HUO HUO.....LORI LAUA WANNE TABORA 30 WAJERUHIWA VIBAYA....


Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Peter Ouma akiangalia Lori aina ya Isuzu lenye nambari za Usajili T829 AHH mara baada ya kuanguka na kusababisha vifoo vya watu wanne na majeruhi zaidi ya 30 katika ajali iliyotokea Tarafa ya Ilolangulu wakati lilipokuwa likienda mnadani huku likiwa limebeba wafanyabiashara wa mitumba pamoja na mizigo mbalimbali.

Tairi la Lori hilo ambalo lilikuwa bovu lilipasuka na kusababisha ajali hiyo mbaya.
Dereva wa Lori hilo Isuzu Bw.Ally Athuman ambaye alikutwa eneo la ajali hiyo mbaya
Baadhi ya wananchi waliofika eneo la ajali wakishuhudia Maiti zilizokuwa zimekusanywa kwenye gari la Polisi muda mfupi mara baada ya ajali kutokea.


Madaktari chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya Kitete mkoani Tabora wakijaribu kuandika majina ya watu waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa.
Kikosi maalumu cha huduma ya kuokoa afya ya majeruhi katika hospitali ya Kitete ambacho kilichukua hatua za haraka na makusudi kushughulikia majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo.

Idadi kubwa ya watu walivunjika miguu na mikono mbali na wale waliopoteza maisha ambao majeraha makubwa walipasuka vichwa na kuumia vifuani.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!