Tuesday, 19 November 2013

YALIYOJIRI JUU YA SAKATA LA ALIYEUA WATU WAWILI NA KUJIUA MWENYEWE KWA RISASI NDANI YA GARI HUKO ILALA JIJINI.

Mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.
Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu nyingine.
Kwa mujibu wake dereva huyo aliendelea kusimulia, alimpeleka jamaa mpaka aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.
Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba, aliendelea kusimulia dereva huyo.
Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari mama mmoja na wadada wawili.
Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol,  kwa mujibu wa dereva taxi huyo  mara baada ya kuona  hivyo ikabidi akimbie.
Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia limpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.
Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.
Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauwaji hayo.


Dereva Aliyekuwa Akiendesha Gari

Mwili Ukibebwa Kuingizwa Kwenye Gari



Jamaa Aliyeuwa na  baadae  Kujiua mwenyewe

ENDELEA KUWA NASI KWA TAARIFA ZAIDI....

PICHA KWA HISANI YA DANCHIBO BLOG.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!