Tuesday, 19 November 2013

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA WAKATI WAKIOGELEA JIJINI DSM.

 
 
Dar es Salaam.Watu watano wamefariki dunia katika matukio tofauti, likiwemo la watu wawili waliokuwa wakiogelea ufukweni mwa Bahari ya Hindi kuzama na kufa baada ya kuzidiwa na nguvu ya maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema Novemba 17 mwaka huu saa 11.30 jioni eneo la Ufukwe wa Ng’onda Kata ya Kigamboni, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Miembeni Vingunguti, Hajira Juma (11) akiwa na watoto kutoka kituo cha yatima Orphans wakiwa wanaogelea, maji yalimzidi nguvu na kuzama.
Kiondo alisema watoto wa kutoka kituo hicho walimtafuta ilipofika saa 12.15 jioni maiti yake ilionekana kandokando mwa bahari hiyo.
Kiondo alisema Chanzo cha kifo chake inasadikiwa ni kutokuwa na ujuzi wa kuogelea na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni.
Katika tukio lingine, dereva wa pikipiki yenye namba T234 CFW ambaye hakufahamika (25) akitokea Polisi Ufundi Barabara ya Kilwa kwenda maeneo ya Bendera Tatu alipofika eneo la Mivinjeni pikipiki yake iliwaka moto kwenye tanki la mafuta.
Kiondo alisema dereva huyo alishindwa kuimudu na kwenda kugonga kwenye gema na kufariki dunia papohapo.
Wakati huohuo, Novemba 17 mwaka huu saa 6.30 mchana eneo la Mbweni Wilaya ya Kinondoni Mkazi wa Masaki Khemi Sunder (57) akiwa anaogelea na wenzake, maji yalimzidi guvu na kuzama.

Kamanda Camilius Wambura alisema wananchi wanaoishi eneo hilo walifanikiwa kumuokoa akiwa hai ambapo walimkimbiza Hospitali ya Ami iliyopo Mikocheni na kubainika kuwa ameshafariki.
Katika tukio lingine lililotokea Novemba 17 mwaka huu saa 2.30 usiku, Mkazi wa Mbezi Makabe aliyekuwa akiendesha baiskeli aligongwa na gari eneo la Mbezi Mwisho na kufariki dunia.

Gari iliyomgonga haikufahamika na marehemu pia hakufahamika jina lake. Maiti imeifadhiwa hospitalini.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!