Miss Universe 2013, Gabriella Isler (25) akiwapungia mashabiki baada ya kutwaa taji hilo mjini Moscow, Urusi usiku wa kuamkia leo.
Miss Universe 2012, Olivia Culpo kutoka Marekani, akimvisha taji la Miss Universe 2013, Gabriella Isler wa Venezuela usiku wa kuamkia leo mjini Moscow, Urusi.
MISS Venezuela Gabriella Isler (25), ametwaa taji la Miss Universe 2013 usiku wa kuamkia leo mjini Moscow, Urusi. Gabriella aliwabwaga washiriki wenzake 85 kutoka mataifa tofauti waliokuwa wanashindania taji hilo. Walioingia Top 5 ni Miss Ecuador, Miss Brazil, Miss Venezuela, Miss Philippines na Miss Spain. Nafasi ya pili katika kinyang'anyiro hicho ilikwenda kwa Miss Spain Patricia Yurena Rodriguez na Mshindi wa tatu alikuwa Miss Ecuador Constanza Baez













No comments:
Post a Comment