WASHITAKIWA 10 wa kesi ya mauaji ya Dr Sengondo Mvungi, leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka lao la kuua kwa kukusudia.
Wakiwa mahakamani hapo, hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa kesi yao itasikilizwa katika Mahakama Kuu. Baada ya kusomewa shitaka lao, washitakiwa walipelekwa rumande hadi Desemba 5, mwaka huu kesi yao itakapo tajwa tena.
Washitakiwa hao ni: Chibago Magozi, John Mayunga, Juma Hamis, Longishu Nosingu, Masenga Mateu, Paulo Mdupha, Nyanela Mlewa, Zacharia Raphael, Msingwa Matonya na Ahmed Kitabu.
PICHA: MUSA MATEJA NA ERICK EVARIST/ GPL













No comments:
Post a Comment