
Rais wa awamu ya tatu Mhe Benjamin Mkapa amesema nchi za Afrika hazitajikomboa kiuchumi kama zitaendelea kutegemea na kushabikia misaada kutoka kwa nchi wahisani na badala yake amezitaka kutambua kuwa kwa kupitia rasilimali na biashara zao wenyewe wanaweza kufika mbali zaidi na wanavyodhani.
Kiongozi huyo ambaye enzi za utawala wake aliamini katika sera yake ya ubinafishaji wa mashirikia ya ummaa ameyasema hapo alipokuwa akishiriki katika kongamano lililowashirikisha pia marais wastaafu Olusegun Obasanjo wa Nigeria na Festus Mogae wa Botswana kongamano ambalo limeandaliwa na taasisi ya uongozi.
Akiunga mkono hoja hiyo mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi Dk Reginald Mengi amezitaka nchi za Afrika kuacha utegemezi na kujibidisha katika kutumia utajiri wa raslimali katika kujikomboa kiuchumi.
Aidha Mh Mkapa amesema bado sekta binafsi nchini hazijawa imara sana na badala yake zimekuwa zikitumia muda mwingi kufanya mikutano, makongamano vikao vya namna ya kufanya biashara badala ya kufanya biashara kwa vitendo.
Kwa upande wake Mh Obasanjo wa Nigeria amesema katika kipindi cha utawala wake alihakikisha kuwa kila jambo lilokuwa linafanywa na serikali yake lililenga kuhakisha kuwa linamsaidia mnaijeria hasa kuanzia elimu hadi kilimo.
Mh Mogae ambaye anatajwa kuwa ni miongomo mwa viongozi bora barani Afrika kutokana na kujizolea tuzo mbalimbali akizungumza katika kongamano hilo amewataka viongozi wa Afrika kusimamia yale wanayoyaamini lakini pia akawatahadharisha kuwa wawe tayari kukokoselewa .
Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na mawaziri na viongozi mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi pamoja na wafanyabiashara maarufu sambamba na mawaziri wakuu wastaafu akiwemo Mh David Cleopa Msuya na Mh John Malechela













No comments:
Post a Comment