Friday, 1 November 2013

LUTENI RAJABU AHMED MLIMA ALIYEFARIKI KATIKA SHUGHULI ZA KULINDA AMANI NCHINI CONGO AZIKWA








Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Mh. Shamsi Vuai Nahodha ameongoza wanajeshi , wakazi wa jiji la Dar es Salaam ndugu na jamaa katika kuaga mwili wa afisa wa jeshi la Tanzania Luteni Rajabu Ahmed Mlima aliyefariki Jumapili  huko jamuhuri ya demokrasi ya Congo- DRC akiwa katika shughuli za kulinda amani.
Mara baada ya mwili huo kuwasili ndege za kijeshi zilionekana zikiruka angani huku vilio Vikirindima kutoka kwa ndugu na jamaa na baadae Mh. Waziri Shamsi Vuai Nahodha aliongoza viongozi mbalimbali wa serikali, mabalozi ,wanajeshi pamoja na waombolezaji Ili kutoa heshima zao za mwisho.
 Aidha waziri Shamsi Vuai Nahodha amesema wamepokea kifo hicho kwa masikitiko makubwa na kubaini tukio hilo halitawakatisha tamaa wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania Kuendelea kulinda amani mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo ili kuhakikisha wanyonge wa nchi hiyo wanaishi kwa amani.
Kwa niaba ya mkuu wa majeshi ya ulinzi jenerali Davisi Mwamunyange, Luteni  jenerali Samweli Albert Ndomba mbali na kusikitishwa na kifo hicho amelezea marehemu alipigwa risasi wakati akikinga raia wa DRC kudhurika wakati jeshi la nchi hiyo wakishambuliana na kikundi cha M23..
Msemaji wa familia ambaye ni kaka wa marehemu amesema marehemu alikuwa ni tegemeo kwa familia yao na kuwa alitarajia kufunda ndoa Disemba mwaka huu na ameacha mtoto mmoja wa kike.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!