Monday, 18 November 2013

HATIMAYE DK SENGONDO MVUNGI AZIKWA WILAYANI MWANGA MKOANI KILIMANJARO


Jeneza lenye mwili wa Dk Sengondo Mvungi likishushwa kaburini.Mwanga, Tanzania. 

Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi amezikwa Leo, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Katika ibada ya mazishi, Askofu Rogath Kimario wa Dayosisi ya Same ya Kanisa Katoliki amesema tukio la kuuawa kwa Dk Mvungi halikuwa tukio la ujambazi bali lilikuwa ni tukio la kimtandao.


Askofu Kimario amesema waliofanya mauaji hayo ni wauaji wa kimtandao na kuitaka Serikali kufuatilia suala hilo na kutoa majibu sahihi kuhusu mauaji hayo


Eti wanasema waliotenda hilo ni majambazi!, nani kasema ni majambazi? Ni research (utafiti) ipi ama upelelezi gani umefanyika. Hawa ni wauaji wa kimtandao,”amesema.


Ibada ya mazishi ya Dk Mvungi ilifanyika Kanisa la Moyo wa Mtakatifu Yesu la Parokia ya Kisangara Juu lilipo Chanjale wilayani Mwanga.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!