Wednesday, 20 November 2013

HABARI ZA KIMATAIFA/ WATU 50 WAANGUKIWA NA JENGO AFRIKA YA KUSINI.



 Watu wawili wamefariki na wengine takriban watu 50 kukwama kwenye vifusi baada ya paa ya jumba la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.
Inaarifiwa watu 29 wameweza kuokolewa.
Madaktari kutoka kampuni ya kibinafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban.
“Shughuli hii itachukua mda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama,” alisema msemaji wa kampuni hiyo.
Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.
Inaarifiwa watu wengine 26 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majereha mabaya.

WAKATI HUOHUO..






Afrika Kusini yasitisha uokoaji kwa muda
 Jitihada za uokoaji zimesitishwa kwa muda baada ya paa la jengo la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.
Msemaji wa Polisi Thulani Zwane ameiambia BBC kwamba kazi ya kuwatafuta watu walionusurika itaanza tena baada ya kuondoa baadhi ya matofali.
 
Mtu mmoja ameripotiwa kufa na wengine 40, wengi wao wakiwa ni mafundi wa ujenzi wanahofiwa kukwama katika kifusi katika eneo la ujenzi la Tongaat, kaskazini mwa Durban.
Watu wapatao 30 wameokolewa, baadhi yao wakiwa katika hali ya taharuki.
 
Kepteni Zwane amesema watu 11 miongoni mwa waliopelekwa hospitali wamejeruhiwa vibaya.
Naibu meya wa mji wa Tongaat ameviambia vyombo vya habari vya Afrika Kusini kuwa serikali ilipata amri ya mahakama mwezi mmoja uliopita, kusitisha ujenzi katika eneo la Tongaat, ambao ni mji mdogo uliopo kilomita 40 kaskazini mwa Durban

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!