skip to main |
skip to sidebar
CHRISTINE AELEZA KISA CHA MAUAJI YA MAPENZI DSM
Dar es Salaam. Imebainika kwamba sababu ya shambulizi la risasi lililotokea
Ilala Bungoni, Dar es Salaam Jumanne iliyopita
na kusababisha vifo vya watu watatu, ni wivu wa mapenzi uliopindukia.
Akizungumza nyumbani kwao Ilala Bungoni jana, mmoja wa majeruhi
ambaye ndiye aliyekuwa kiini cha shambulizi hilo
Christine Newa alisema si kweli kwamba sababu ya mchumba wake
Gabriel Munisi kuwashambulia na kuwajeruhi
kwa risasi yeye na mama yake mzazi, Ellen Eliezer na kumuua mdogo
wake wa kike, Alpha Newa ni kutokana na kusaliti
uchumba wao.
Awali, ilidaiwa kwamba sababu ya shambulizi hilo ni Christine kumkataa
Munisi, (ambaye pia alijiua baada ya kufanya
mauaji hayo) na kuchumbiwa na rubani wa ndege, marehemu Francis Shumila
ambaye pia alifariki katika tukio hilo.
.. “Kwanza Shumila hakuwa mchumba wangu kama ilivyoelezwa.
Alikuwa shemeji yangu, mume wa dada yangu Caroline Newa.
Pia hakuwa rubani wa ndege, bali nahodha wa meli.”
Alisema amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Munisi katika kipindi
kisichofikia mwaka mmoja lakini sehemu
kubwa ya maisha yao ikitawaliwa na misuguano iliyowafikisha polisimara kadhaa.
Alisema katika kipindi cha uhusiano wao marehemu Munisi alikuwa
akimpiga, akimkataza kufanya kazi, kusoma
na alikuwa na wivu uliopindukia.
Christine kuona hivyo, aliamua kufanya mipango ya kwenda kusoma
katika Visiwa vya Cypruskimyakimya pasi
na kumuaga, jambo ambalo alisema lilimkera mchumba wake huyo na kuweka
kisasi.
“Nikiwa huko, Munisi alitafuta mawasiliano hadi akayapata
na tukawasiliana.
na siku niliporejea alikuja kunipokea
uwanja wa ndege lakini cha ajabu, alinikataza kwenda nyumbani na badala yake akanipeleka moja kwa moja hadi Mwanza
eneo la Kitangiri,” alisema na kuongeza: “Tukiwa njiani kuelekea
Mwanza, katika maeneo ya Singida,
alisimamisha gari akaniambia nishuke, akatoa bastola na kuniuliza
kwa nini niliondoka bila ya kumuaga. Je, nataka kumuacha?”
Alisema alimwomba msamaha na kuendelea na safari yao. Anasimulia
kwamba baada ya kufika Mwanza, alimpora simu zake zote
na kumfungia ndani kwa zaidi ya wiki mbili hadi alipopanda kwenye
dirisha na kuomba msaada kwa majirani
na kuwapa namba za simu za ndugu zake ili wamsaidie kuwapa taarifa.
Ndugu zake walianza mchakato wa kuwasiliana na polisi hatua iliyofanikisha
msichana huyo kurudishwa Dar es Salaam...
“Hata hivyo niliondoka na khanga na fulana tu. Vitu vyote niliviacha huko.”
Baada ya kurudi Dar es Salaam, anasema Munisi naye aliamua kumfuata
lakini safari hii alifikia katika Hoteli ya MM iliyotenganishwa na ukuta
wa nyumba yao na akawa anafuatilia nyendo za familia hiyo.
“Alikuwa ananitumia meseji kwamba amemuona dada Caro, mama na Alpha
na wakati mwingine anasema ameniona mimi mpaka nguo tulizovaa, tukaanza
kupata na wasiwasi,” alisema.
Wasiwasi huo ulitokana na historia ya maisha yao ya Mwanza na pia tishio ambalo
anadai kwamba Munisi aliwahi
kulitoa kwamba atahakikisha anaiteketeza familia yote kuanzia Goba anakoishi
mama yake (Ellen), Zanzibar anakoishi
mdogo wake (marehemu Alpha) na hapo Ilala.
Anasema walikwenda polisi lakini walielezwa kwamba hayo ni masuala madogo ya mapenzi
na kwamba yatamalizwa kifamilia.
Siku ya tukio Christine alikuwa akitoka kwenda uwanja wa ndege tayari kwa safari
ya kurudi shuleni Cyprus
ndipo Munisi alipotokea na kuanza kumrushia Shumila risasi na baadaye Alpha
kisha mama na yeye kabla ya kujiua.
Akizungumzia tukio hilo, Caroline alisema mumewe alitabiri kifo chake kabla kwani baada
ya kusikia vitisho vya Munisi
, alimtoa shaka Christine akimwambia kwamba atamlinda hata ikibidi kupoteza maisha yake, jambo ambalo lilidhihiri.
Alisema mama yake amepata nafuu na ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili alikokuwa amelazwa na mazishi ya mdogo wake, Alpha ambaye ameacha
mtoto mwenye umri wa miezi minane, yamepangwa kufanyika Jumamosi
Goba, Dar es Salaam.
Alisema mipango ya mazishi ya mumewe inafanywa huku akidokeza kwamba huenda
akasafirishwa kwenda Mombasa.
chanzo:mwananchi
No comments:
Post a Comment