Friday 18 October 2013

WASICHANA WA KINGEREZA WALIOMWAGIWA TINDIKALI HIVI KARIBUNI VISIWANI ZANZIBAR, KUREJEA TENA TANZANIA MWAKA 2014.


 

1RAIA wawili wa Uingereza waliomwagiwa tindikali visiwani Zanzibar miezi mitatu iliyopita, wamepanga kurejea tena visiwani humo kuendelea na kazi za kujitolea ikiwemo kuwahi kuhudumia watu wasiojiweza.
Raia hao wa Uingereza, Kirstie Trup na Katie Gee, hivi sasa wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali za Chelsea na Westminster London na taarifa zinaeleza kuwa afya zao zimeimarika kwa kiwango cha kuridhisha hasa baada ya kufanyiwa upasuaji na kisha kuwekewa ngozi upya.
Pamoja na madhara waliyokumbana nayo raia hao wamesema kuwa bado hawajakatishwa tamaa na tukio hilo na sasa wanapanga kurejea tena visiwani humo kuendelea na kile walichokiita ‘kazi za upendo’.
Katika waraka wake uliochapishwa na Gazeti na Daily Telegraph, Kirstie Trup amesema kuwa yeye na mwenzake wamepanga kurejea Zanzibar mwaka ujao na kwamba safari hii wataongeza kasi ya kushiriki kazi za kujitolea.
“Kwa sasa tuko imara na mwakani tumepanga kurejea tena visiwani Zanzibar kushiriki katika kazi za kujitolea,” alisema Trup ambaye ngozi yake imefanyiwa ukarabati wa kisayansi na kuwekewa ngozi upya katika eneo la mkono wa kulia na sehemu ya bega.
Akielezea zaidi kuhusiana na tukio hilo la kumwagiwa tindikali, Trup alisema kuwa anachokumbuka ni kuwa wakati akiwa na mwenzie wakielekea mgahawani ghafla walijitokeza watu wawaili na walipowakaribia walichomoa kopo kutoka kwenye mfuko na kumwaga kitu cha majimaji ambacho baadaye kilibainika kuwa ni tindikali.
“Mwili mzima uliwaka kama vile nimechomwa na moto. Maumivu yalikuwa makali sana yasiyoweza kuelezeka hasa katika eneo la bega langu la kulia. Nachokumbuka kingine ni kuwa tulipiga kelele kwa sauti sana hata kufanya wale waliokuwa kwenye hoteli iliyokuwa jirani na sisi kutahamaki,” alisema Trup.
SOURCE;JUMA MTANDA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!