Saturday 19 October 2013

SIKU CHACHE ZILIZOPITA NILITOA HABARI KAMA HII AMBAYO ILINIKWAZA KUPITA ZOTE LEO TENA NAKUTANA NA HII NYINGINE, NANI WA KWENDA JELA MWIZI AU WEWE ULIYEUA? TUBADILIKE JAMANI!

INATISHA SANA KWA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI...MWIZI APIGWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI NA KUFA PAPOHAPO HUKO MBAGAL JIJINI DAR..

 


Picha hii nikimuhoji Marehemu Boni kabla hajafariki dunia!

Kijana mmoja anaefahamika kwa jina la Boni amefariki dunia kutokana  na kupigwa na wananchi wenye hasira baada ya kukutwa akiwa anaiba mbao ambazo zinatumika na mafundi kuwekea linter (linta)


samahani picha zingine mtakazo ziona zinahitaji moyo!

Tukio hilo lililotokea jana Ijumaa saa 3 asubuhi maeneo ya nzasa eneo maarufu kama bonde la kwa Sanvu  kijana huyo alikutwa na mkasa huo alipokua akijaribu kuiba mbao ambazo zilikua zinatumika na Mafundi kufungia linter kwenye nyumba ndipo alipo bambwa na mwenye nyumba hiyo ambae jina tunalihifadhi alipopiga kelele za kutaka msaada uliasababisha wananchi wakimbilie eneo la tukio.

 wananchi hao wakaamua kuchukua sheria mkonononi licha ya kuonywa sana juu ya kuchukua sheria mikononi wakampiga, lakini kitu kilicho sababisha marehemu akutwe na maafa hayo ni kua alikamatwa eneo la katikati ambalo linagawanya maeneo mawili tofauti yani eneo la Nzasa na eneo la Maji matitu alivyokamatwa na wananchi wa nzasa walimpiga wakamuachia na kumwambia aondoke eneo hilo na asirudi tena wakati Marehemu anaondoka likatokea kundi kubwa la wananchi wa Maji matitu ambao walikua na hasira kwamba angalau leo wamempata mwizi anaewatobolea madirisha yao na mwizi wa vitu vyao kipigo kikaanza upya! ikabidi wananchi wa nzasa waanze tena kumuombea msamaha ili asije akafia maeneo ya kwao, kwa juhudi za wananchi wa nzasa walifanikiwa kuwatuliza wananchi wa Maji matitu  ndipo mwandishi wa habari hizi alipo pata nafasi ya kumuhoji Boni je ni kweli ulikua umekuja kuiba?

 Boni alilikiri mbele yangu kua kweli alifika eneo husika kwa ajili ya kuiba, ikabidi muandishi apige simu polisi ili wajwe wamchukue Bonikabla raia hawajaamua vingine wakati Marehemu Boni baada ya kuhakikishiwa kua hatapigwa tena na  alijitahidi aondoke eneo hilo la tukio ndipo alipoishiwa nguvu na kudondoka kwenye choo kilichokua jirani na eneo hilo ambapo alikaa mpaka Asksri polisi walipofika lakini wakati wanataka kumuhoji Marehemu Boni alifariki dunia

 


                 Marehemu Boni akiwa amedondokea Chooni 


                 

   BONI AKIWA TAYARI AMEPATWA NA UMAUTI  



Kijana huyo ambae Baba yake ni Askari Polisi  na ni kijana anaetoka katika familia inayojiweza atazikwa leo huko maeneo ya Mbagala kwa wa mbili



 USHAURI WA "VITUKOVYAMTAANEWS.COM" KWA WASOMAJI..



Wananchi tuache kuchukua sheria mikonononi kwa kua pale yule anakua ni  mtuhumiwa hakuna chombo chochote cha sheria ambacho kitakua kimemthibitisha kwamba ni muhalifu pia wewe ndie utakua umetenda kosa kubwa na lenye adhabu kubwa kuliko huyo unaemuhukumu mfano wa tukio hili Boni alitaka kuiba mbao wewe umeua! nani anaepaswa kushitakiwa na kufungwa?? 



tubadilike tufuate sheria bila shurti , Jeshi la Polisi lipo kwa ajili yetu tuliamini ili tujenge amani yetu......

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!