Pages

Monday, 21 October 2013

SHABIKI SIMBA ASHANGILIA BAO LA NGASSA, APATA KIPIGO KITAKATIFU, WENGINE 21 WAZIMIA JUU YA MECHI YA JANA

 

Mmoja wa mashabiki wa Yanga waliozimia.
Na Martha Mboma
SHABIKI mmoja wa Simba jana alikiona cha moto baada ya kushangilia bao lililofungwa na Mrisho Ngassa wa Yanga.
Ngassa alifanikiwa kuifungia timu yake ya Yanga bao la kwanza kwenye mchezo wa jana dhidi ya watani wao wa jadi Simba katika dakika ya 15 kipindi cha kwanza.
Mara baada ya bao hilo, shabiki huyo wa Simba ambaye alikuwa katikati ya mashabiki wenzake, alipandwa na mzuka na kushangilia kwa nguvu hali ambayo ilizua tafrani kubwa.
Baada ya shabiki huyo kushangilia, wenzake walimgeukia na kuanza kumpa kipondo cha hali ya juu lakini askari waliokuwa uwanjani hapo walikimbilia eneo la tukio na kumuokoa huku akiwa ameshapata kichapo cha hali ya juu.
Wakati huohuo shabiki mmoja wa Yanga alizimia baada ya Ngassa kufunga bao hilo. Shabiki huyo aliyekuwa jukwaa la Yanga, alizimia kwa furaha na watu wa huduma ya kwanza walikwenda haraka kwenda kumtibu.
Hata hivyo hali hiyo iliendelea kile bao lilipokuwa likifungwa na hadi Hamis Kiiza anafunga bao la tatu, mashabiki saba wa timu hiyo walikuwa wameshazimia na kubebwa na machela. Inaelezwa kuwa, jumla ya mashabiki 21 wa Yanga na Simba walizimia jana

No comments:

Post a Comment