Pages
▼
Monday, 21 October 2013
RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI MKOA WA NJOMBE
Rais Jakaya Kikwete akiambatana na Mkewe Mama Salma Kikwete wakipokea taarifa fupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mufindi Tea Company Group Bwana Noel Smith, kuhusu kukamilika kwa kiwanda cha chai walichokijenga katika kijiji cha Ikanga kilichoko katika Kata ya Lupembe, wilayani Njombe ambacho Rais Kikwete alikizindua rasmi tarehe 18.10.2013
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiangalia majani ya chai yaliyofikishwa katika kiwanda cha chai cha Ikanga kwa ajili ya kusindikwa. Kiwanda hicho kilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 18.10.2013.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiangalia chai iliyosindikwa na kufikia hatua ya mwisho kabla ya kufungwa kwenye pakiti huku wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha chai cha Ikanga Bwana Flowin Msigwa .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia mamia ya wananchi wa kijiji cha Wanginyi kilichoko katika kata ya Lupembe, wilayani Njombe kwa kuwapungia mikono mara baada ya Mama Salma na Rais Kikwete kuwasiri kijijini hapo kwa ajili ya mkutano wa hadhara tarehe 18.10.2013
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na akinamama wa kikundi cha Jitegemee wakati wa maonyesho yaliyofanyika mjono Njombe kwa ajili ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa wa Njombe huku kiongozi wa kikundi hicho Mama Leokadia Kaduma akimfafanulia juu ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanakikundi hao
Chipukizi wa Mkoa wa Njombe wakicheza halaiki wakati wa sherehe ya ufinguzi rasmi wa Mkoa wa Njombe zilizofanyika tarehe 18.10.2013
Rais Jakaya Kikwete akibonyeza king’ora huku wazee wawili wa kimila wakiwa wamewashika njiwa na baadare kuwarusha hewani kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa mkoa wa Njombe katika sherehe zilizofanyika mjini Njombe tarehe 18.10.2013
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment