Pages

Wednesday, 23 October 2013

SAMAKI WALIOHARIBIKA WALIOINGIZWA TOKA CHINA WATEKETEZWA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA.


  • Samaki walioingizwa nchini toka China wameteketezwa na TFDA. Kwa taarifa zaidi bofya-> http://bit.ly/18ces8K



Samaki walioingizwa nchini na kuanza kuuzwa mitaani wakitokea China na kukamatwa wakiwa wameharibika wameteketezwa na mamalaka ya chakula na dawa katika eneo la dampo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Samaki hao aina ya vibua ambao waliingizwa hapa inchini mwezi julai 2013 na kampuni ya Sais Boutique ya bwana Sadick Maporo na kuhifadhiwa katika kontena iliyopo eneo la Tabata bima jijini Dar es Salaam huku zikiwa zinauzwa tayari mitaani ikiwemo katika baadhi ya masoko ya hapa jijini,kabla ya kukamatwa na TFDA mnamo tarehe 18 Septemba 2013 zikiwa zimeoza zimeteketezwa huku mkaguzi wa chakula kutoka TFDA Bi Noor Meghji akieleza hatua zilizochukuliwa na mahakama ya jiji.
Kutokana na mshitakiwa huyo kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni moja tu pamoja na kuteketezwa kwa mali yake ambayo ni zaidi ya tani kumi ya samaki hao zenye thamani ya shilingi milioni kumi na moja,waandishi wa habari walilazimika kumuuliza mwendesha mashtaka wa mahakama ya jiji bwana Ruiza Chrispian kuhusu udogo wa adhabu hiyo ukilinganisha na ukubwa wa madhara ambayo yangeweza kutokea kupitia samaki hao huku mwakilishi wa mmiliki wa samaki hao bwana David Lihenga amekiri kukubaliana na maamuzi ya mahakama ya kuteketeza samaki hao ili kunusuru maisha ya watanzania.
Samaki hao aina ya vibua waliingizwa nchini tangu mwezi julai 2013 na Sais Boutique ya bwana Sadik Maporo zikitokea China katika kampuni ya Frozen Pacific Mackerel scomber japonicus frozen fish zikiwa zimeharibika na zikahifadhiwa katika eneo ambalo halikuwasajiliwa kisheria na tfda kwa lengo la kuuzwa wakati samaki hao ni wabovu na wameoza ambayo kwenda kinyume na sheria ya chakula na dawa na vipodozi ya sura ya 219.

No comments:

Post a Comment