Friday, 18 October 2013

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA RASMI MKOA WA NJOMBE LEO

 
'
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe huku wazee wa Njombe wakirusha njiwa kuashiria kuzinduliwa rasmi mkoa wa Njombe leo Oktoba 18, 2013 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe. PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Maisha Bora kwa Watanzania hajawezi kuja kwa watu kushinda wanacheza mchezo wa pool badala ya kujihangaisha kwa kufanya kazi na shughuli nyingine za kujiingizia mapato.

Aidha, Rais Kikwete ameahidi kuwa Serikali yake itakomesha haraka iwezekanavyo kero ya wananchi wa sehemu za Mkoa wa Njombe kulazimika kupanda mitini ili kupata mawasiliano ya simu za mkononi.

Rais Kikwete amayesema hayo leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Wanginyi, Kata ya Lupembe, Wilaya ya Njombe katika Mkoa Mpya wa Njombe kwenye siku yake ya kwanza katika ziara yake ya siku saba kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo.
 HABARI KWA HISANI YA ISA MICHUZI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!