Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Saimon Gamaya , mwenye umri wa miezi 11 na nusu akiwa na Mama yake Vumilia Ernest aliyelazwa katika jengo la wodi ya watoto akiwa anaumwa sikio na kuharisha. Jengo hilo lilifunguliwa rasmi na Mama Salma tarehe 15.10.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
………………………………….
Na Anna Nkinda- Maelezo, Iringa
15/10/2013 Wanawake mkoani Iringa wametakiwa kuitumia Hospitali ya rufaa ya mkoa huo kupata huduma ya uzazi pamoja na watoto wao na kuachana na tabia ya kujifungulia majumbani, kupeleka watoto kwa waganga wa jadi kwa kudhani kuwa magonjwa wanayoumwa hayawezi kutibika Hospitalini.
Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akifungua jengo la huduma za watoto katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambayo imejengwa kwa msaada wa Hospitali rafiki ya Vicenza iliyopo katika mkoa wa Veneto nchini Italia.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuna baadhi ya wazazi wakiona watoto afya za watoto wao zinadhoofika ikiwa ni pamoja na kuumwa ugonjwa wa utapiamlo wanadhani kuwa jirani zao wanawaonea wivu na kuwaroga na wanaona njia sahihi ni kwenda kwa waganga wa jadi badala ya kuwapeleka Hospitali ili wakaonane na wataalamu wa afya.

Alisema vifo vya watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa sasa ni 54 katika kila watoto wanaozaliwa wakiwa hai 1000 na katika mkoa huo idadi ya vifo hivyo ni watoto 20 kwa kila vizazi hai 1000 nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vifo hivyo vinapungua ili kuweza kufikia malengo ya Maendeleo ya Milinia ifikapo mwaka 2015.
Aidha Mama Kikwete pia aliwataka wakazi wa mkoa huo kujiepusha na mazingira yawatayowapeleka kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kuwa waaminifu katika ndoa zao na kwa wale ambao hawana ndoa watulie na kujitunza huku wasubiri muda wao wa kuoa au kuolewa ukifika.
“Mkoa huu maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) yako juu takwimu zinaonyesha kuwa watu tisa kati ya 100 wanamaambukizi , hivyo basi nawasihi mjitunze na kuheshimu ndoa zenu kwa kufanya hivyo hamtaweza kupata maambukizi ya ugonjwa huu kirahisi ingawa unaweza ukapata kwa njia nyingi lakini maambukizi mengi yanapatikana kwa njia ya kufanya mapenzi yasiyo salama”, alisema Mama Kikwete.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma aliushukuru uongozi wa mkoa wa Veneto na Hospitali ya Vicenza kwa msaada wa ujenzi wa wodi ya watoto na ujenzi wa jengo la kujifungulia kina mama wajawazito.
Dkt. Ishengoma aliahidi atahakikisha na kusimamia ili jengo hilo liweze kutumika kama lilivyokusudiwa na wahudumu wa Hospitali hiyo waweze kutoa huduma bora kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.

No comments:
Post a Comment