TUNAOMBA RADHI KWA VIDEO HII
Albugas Shiyo, 41, ameuawa kikatili na madereva wa Bajaj na wa pikipiki maarufu kama Bodaboda, baada ya kuitiwa mwizi na dereva wa Bajaj iliyomgonga na kukataa kumpeleka hospitalini.
Tukio hilo lilitokea Chang’ombe Maduka Mawili, Temeke jijini Dar es Salaam hivi karibuni, wakati marehemu akiwa na wenzake wakitokea katika shughuli zao Kigamboni Wilaya ya Temeke jijini Dar.
Mauaji hayo yamewachanganya wakazi wa eneo hilo ambalo inadaiwa kwa kipindi kirefu hakujawahi kutokea uhalifu na wamefadhaika kwa kuwa aliyeuawa ni mtu ambaye alikuwa anaishi katika eneo hilo kipindi cha nyuma kabla ya kuhamia alikojenga, Majohe, Ilala jijini hapa.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa marehemu ambaye kazi zake zilikuwa ni fundi ujenzi, alikuwa akitoka kazini akiwa na wenzake wawili waliotajwa kwa jina mojamoja; Zahoro na Baba Mwalimu wakitokea katika ‘saiti’ ya ujenzi Kigamboni.
“Walipofika katika maeneo ya Keko wakiwa wanatembea kwa miguu, Shiyo aligongwa na Bajaj na kuumia mkono wa kushoto, akamuambia dereva aliyemgonga kuwa ampeleke hospitali kwa kuwa amemuumiza,” kilisema chanzo chetu eneo la tukio.
Inadaiwa kuwa dereva huyo aliyetajwa kwa jina moja la Omary, alikataa kumpeleka hospitali na kukatokea mabishano kati yake, marehemu na wenzake aliokuwa nao ambao waling’ang’ania kwenye Bajaj lakini dereva aligoma.
Hata hivyo, dereva huyo aliamua kuondoka nao hadi katika kituo chake cha kazi, akawageuka na kuanza kupiga yowe kuwa watu hao ni wezi wanataka kumnyang’anya Bajaj yake, ndipo madereva Bodaboda walipojitokeza kwa wingi na kuanza kuwapiga.
“Wenzake walifanikiwa kukimbia lakini yeye kwa kuwa alikuwa tayari majeruhi wa mkono alishindwa, akapigwa hadi akaishiwa nguvu,” alisema shuhuda huku akiomba jina lake kuhifadhiwa.
Alisema baada ya madereva kuona Shiyo ameishiwa nguvu, walianza kumpanda mmoja baada ya mwingine kwa pikipiki zao hadi walipohakikisha amekufa, wakatafuta tairi na petroli kisha wakamchoma moto.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili huku wakiomba majina yao kutoandikwa gazetini kwa kuhofia usalama wao, walisema kuwa kijana aliyemgonga marehemu ni mtu wa matukio na baada ya tukio hilo alikuwa anatamba mtaani kuwa amemfanyizia marehemu na hakuna mtu atakayemfanya kitu.
“Ni kawaida kwa madereva wa Bajaj au pikipiki kuvamia hata madereva wa magari wanapofanya makosa na kujichukulia uamuzi wa hata kulichoma gari wakati pengine makosa wamefanya wao.
“Wengine ni wezi, akina mama wengi wameporwa mabegi yao na hawa madereva wa bodaboda, ingefaa viongozi wa serikali wakavalia njuga hili tatizo,” alisema mtu mmoja.
Daktari mmoja wa Hospitali ya Temeke alisema marehemu aliungua kwa asilimia 90, hali iliyosababisha apoteze maisha.
“Hawa watu walidhamiria kumuua kwa sababu nimeambiwa walimvisha tairi shingoni na kumchoma kama kibaka,” alisema daktari huyo aliyesema asiandikwe jina kwa kuwa siyo msemaji wa hospitali.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP Englebert Kiondo alipohojiwa, alisema: “Tukio hilo lipo na liko katika uchunguzi. Hadi sasa tunamshikilia mtu mmoja kuhusiana na mauaji hayo.”













5 comments:
HAWA NI WAKUNYONGWA KABISA
Everything is very open with a very clear description of the issues.
It was really informative. Your site is very useful.
Thank you for sharing!
My web blog: baby gender predictor
Hello, I read your blog like every week. Your humoristic style is awesome, keep it up!
Here is my website :: soci vidz evaluations
It's going to be ending of mine day, however before end I am reading this wonderful
post to improve my know-how.
Feel free to visit my web blog :: soci video evaluations
This info is worth everyone's attention. When can I find
out more?
Feel free to surf to my weblog :: Ricky Salvador
Post a Comment