Wednesday 4 September 2013

SERIKALI YATISHIA KUUSHITAKI MTANDAO WA KENYA KWA KASHFA


                                   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assa Mwambene  
Serikali imetishia kuuchukulia hatua za kisheria, ikiwamo kuushtaki mahakamani mtandao wa Standard unaomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya The Standard ya nchini Kenya, kwa madai ya kuidhalilisha Tanzaniakwa kuionyesha haiko makini na Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kutokana na kitendo hicho, imeutaka mtandao huo wa www.standardmedia.co.ke kuiomba radhi Tanzania, vinginevyo, itauchukulia hatua hizo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assa Mwambene, alisema wako kwenye mchakato wa kuwaandikia wamiliki wa mtandao huo barua, kuwataka watekeleze suala hilo mara moja.

Mwambene alisema hayo baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kujibu taarifa iliyotolewa na mtandao huo Septemba mosi, mwaka huu.

Alisema taarifa ya mtandao huo inaonyesha kwamba, Tanzania haiko makini na EAC, ikiwa ni pamoja na kukwamisha jitihada zinazofanywa na Kenya kuimarisha ushirikiano huo.

Kwa mujibu wa Mwambene, taarifa ya mtandao huo inadai kuwa jengo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) lilipoungua moto mwezi uliopita, baadhi ya nchi zilizoko EAC zilisaidia kwa kuruhusu ndege kutua katika viwanja vyake, lakini Tanzania ilikataa.

Alisema mtandao huo umedai pia kuwa miaka miwili iliyopita, Kenya walipokabiliwa na baa la njaa, waliiomba Tanzania iwauzie chakula (mahindi), ikawanyima, lakini ikaiuzia Uganda.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!