Tuesday, 17 September 2013

JE WAFAHAMU HISTORIA YA MJI WA KIGOMA?

   

Mkoa wa Kigoma katika Tanzania
Kigoma iko kati ya mikoa 26 za Tanzania. Imepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa la Tanganyika penye mpaka na Kongo
 
Mnamo Machi 2012 zimeongezwa wilaya mpya za Buhigwe, Kakonko na Uvinza.
Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu.
Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye UB wa 800m karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750.
Mito ya kudumu ndiyo Malagarasi, Luiche na Ruchugi
Kuna wilaya nne ndizo (idadi ya wakazi katika mabano): Kigoma Mjini (144,852), Kigoma Vijijini (490,816), Kibondo (414,764) na Kasulu (628,677). Jumla ya wakazi ni 1,679,109 (sensa 2002). Makao makuu ndipo Kigoma mjini.


Wakazi

Kabila kubwa ni Waha, likifuatiwa na Wamanyema. Kuna pia Wabembe, Wanyamwezi, Wasukuma, Wafipa na watu wenye asili ya Kongo, Rwanda na Burundi.
Idadi au msongamano wa watu katika maeneo ya mkoa huu imetegemea sana kupatikana kwa nzi aina ya ndorobo: penye ndorobo wengi watu ni wachache.

Uchumi na mawasiliano

Mkoa wa Kigoma haukuona bado maendeleo yanayolingana na mazingira yake. Hali ya barabara na mawasiliano mengine ni mbaya. Umbali hadi Daressalaam ni 1316 km, hadi Mwanza 830 Km, hadi Arusha 1204 Km. Lakini hakuna barabara ya lami hata barabara za kokoto ni sehemu ndogo to.
Usafiri muhimu ni reli ya kati kutoka Kigoma kwenda Daressalaam kupitia Tabora na Dodoma. Isipokuwa reli hii imeshazeeka ilhali imejengwa zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Treni zake huchelewachelewa zinachukua muda mrefu. Wakati wa mvua inatokea ya kwamba mawasiliano yanavurugika.
Uwanja wa ndege wa Kigoma inashughulika ndege ndogo aina ya Fokker.
Mnamo 85% ya wakazi wote hutegema kilimo, walio wengi kilimo cha kujitegemea tu.
Kuongezeka kwa wakimbizi kutoka nchi jirani na kukua kwa makambi kulikuwa tatizo kubwa.

Hifadhi za wanyama na za kihistoria

Kuna maeneo mawili penye sokwe: ndipo Hifadhi ya Taifa ya Gombe (alikofanya utafiti wake mwanabiolojia Jane Goddall) na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale.
Mji wa Ujiji ulioko karibu na Kigoma mjini ndio mji wa kale zaidi katika Tanzania ya Magharibi penye makumbusho wa Dr. Livingstone


Kituo cha reli cha Kigoma
Mji wa Ujiji ulioko Magharibi mwa Tanzania una historia ndefu miongoni mwa miji ya kale ya Afrika Mashariki na Kati ukihusishwa na biashara ya watumwa kutoka Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Ni katika eneo hilo la Ujiji ndiko mvumbuzi wa kimataifa, Dr David Livingstone, alipofikia akiwa katika safari zake zilizomtoa pwani ya Afrika mashariki hadi Kongo. Kwa sasa kuna makumbusho maalum kwa heshima yake na kumbu kumbu ya vizazi vijavyo.
 Lakini nusu karne baada ya uhuru wa Tanzania, umaarufu wa mji huo mkongwe umeporomoka na hali ya maisha ya watu wake imeendelea kuwa duni. Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ametembelea mji huo na kujionea hali ilivyo. 
Kwenye kituo cha makumbusho ya Dr David Livingstone katika eneo la Mnazi Mmoja-Kabondo Ujiji ni eneo ambalo kuna majengo mazuri yenye vyumba kadhaa vilivyobeba alama za ujio wa Mvumbuzi huyo aliyechangia kukomeshwa kwa biashara ya utumwa, lakini pia kumbukumbu za asili za vitu na watu wa mji huo.
Kufifia kwa umaarufu wa eneo kongwe la Ujiji kulichangiwa na sababu nyingi, ikiwemo kuanzishwa kwa mji mpya wa Kigoma. Kurejea kwa Ndiyunze Msherwampamba aliyekuwa kiongozi wa watu wa kabila la wagoma kutoka Kongo kuliibua jina la mji mpya Kigoma.
 Alhaj Mikdad bin Ibrahim Tawfiq Malilo mwenye miaka 79 mkaazi maarufu wa Ujiji, ameiambia BBC kuwa Msherwampamba alipokelewa pamoja na wafuasi wa kabila lake na wakapewa eneo la kujitawala ambalo wakati huo lilikuwa likiitwa Rusambo , na sasa ndilo linaloitwa Kigoma.
 „Walipompokea Msherwampamba wakapewa kanchi, eneo lenyewe ni sehemu hivi sasa wanasema ikulu ndogo zamani tulikuwa tunasema Kaizahofu, eneo lote lile kabla ya hapo lilikuwa linaitwa Rusambo.
Sasa wenyeji warundi ndiyo wanajiita wajiji wakawa wanakwenda kuwatembelea wanasema 'tugende kubagoma,' likaendelea likabadilika ndiyo ikawa Kigoma basi ndiyo kitovu cha mahala kuitwa Kigoma asili Rusambo”
Kwa miaka mingi nguvu za kiuchumi za wakazi wa mji huo imekuwa ikitegemea Ziwa Tanganyika kwa uvuvi na usafiri wa kwenda na kutoka maeneo mbali mbali ya mwambao wa ziwa hilo zikiwemo nchi jirani za Burundi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Pamoja na kupoteza uimara wake, Mji wa Ujiji na Kigoma kwa ujumla umeibuka upya katika miaka ya karibuni kwa kutoa watu waliojipatia umaarufu mkubwa katika eneo lote la Afrika Mashariki na kati ikiwa ni pamoja na wasanii wa muziki wakiwemo Naseeb Abdul anaejulikana zaidi kama Diamond, Wanasoka wastaafu Kitwana Manara, Kassim Manara, Edibily Lunyamila na hata nahodha wa sasa wa Timu ya Taifa ya Tanzania Juma Kaseja .
Tangu enzi za Ukoloni watu kutoka maeneo mbalimbali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Burundi, Rwanda na Zambia waliingia mji wa Ujiji hasa kipindi cha utawala wa biashara ya watumwa

1 comment:

Livingstone M. Batawe said...

Safi sana nimeipenda, ila mm nilikuwa naomba kujua neno #kigoma lilitokana na nn.Asante.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!