Ikiwa bado tukio la shambulizi la woga wa kigaidi,likishughulikiwa na vyombo vya usalama nchini Kenya,idadi ya waliopoteza uhai katika tukio hilo ambalo linachukua zaidi ya Saa 48, imefikia 69 na majeruhi kubaki katika idadi ile ile ya watu 175.
Pamoja na kupokea,salamu za pole na matamko ya kupokea msaada wa kumalizana na tukio hilo,RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta anasema swala hilo kwa sasa Ni la WAKENYA na lipo chini ya vyombo vya usalama wa Kenya,huku akiwathibitishia raia wake kuwa wahusika wa tukio hili watadhibitiwa na kushuhhulikiwa inavyostahili.
Muda mchache uliopita milio ya risasi iliendelea kusikika kutoka eneo la tukio, ambapo inadaiwa washambuliaji hao waoga idadi yao inafikia kuwa kumi mpaka kumi na tano
Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya huku mateka wakinusuriwa
Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao..
. Pia anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wanpokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwawa magaidi wawili
Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao
Nae Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti hali na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka.
.

No comments:
Post a Comment