Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Askari mwenzao, Marehemu Private, Hugo Munga alifariki dunia Septemba 18 mwaka huu huko Pretoria Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata akiwa na vikosi vya MONUSCO Congo DRC katika operations ya kuwaondoa waasi wa M23. Mwili wa Munga ulisafirishwa jana kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu ilifanyika Viwanja vya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam.
Mama wa Marehemu, Jovitha Barnaba Munga akisaidiwa kuaga mwili wa mwanae.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza
Viongongozi mbalimbali wa Siasa na Jeshi wakiwa katika shughuli hiyo.
No comments:
Post a Comment