Tuesday 16 July 2013

WITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KILA MWEZI KUFUATIA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2013

WITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KILA MWEZI KUFUATIA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2013

Sisi wananchi wa Tanzania:
• Tukiwa ni wapiga kura wa majimbo mbalimbali nchini Tanzania, tumechukua jukumu leo kutoa wito kwa wabunge na serikali kufuta tozo/kodi mpya ya laini za simu iliyoanza kutumika baada ya sheria kupitishwa na Bunge Juni 2013.
• Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea maendeleo endelevu nchini kwetu.
• Bila mjadala mpana na mawazo chanya yaliyochambua masuala kwa undani kama msingi wa maamuzi, nchi itafanya maamuzi dhaifu yasiyosimama kwenye misingi ya hoja na ukweli wa mambo.
• Kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linakandamiza wananchi na huenda likaturudisha nyuma kimaendeleo, ni kushindwa kuwajibika kama wananchi

Kodi ya kila mwezi kwa laini za simu nchini ni kandamizi kwa wananchi walio wengi hasa vijijini, inarudisha nyuma ukuwaji wa sekta ya mawasilino nchini, ni sekta muhimu inayotakiwa kukuzwa, huduma za muhimu na zinatakiwa kupatikana kwa wananchi wote na kwa unafuu.

KWA SABABU:- Kodi hii inamkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya chini ambao ni 67% ya wananchi wanaoishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs 2,000) kwa siku. Takwimu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za simu milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi. Kuwaongezea mzigo wananchi hawa kwa kiwango ambacho tayari wanashindwa kumudu ni kuwanyima kabisa fursa ya kutumia huduma hii muhimu

CHANZO AVAAZ.ORG

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!