skip to main |
skip to sidebar
SHERIA YA MADALALI KUFANYIWA KAZI......MADALALI WASIOSAJILIWA KUKIONA..
SERIKALI imesema inaandaa taratibu za kuifanyia marekebisho Sheria ya Madalali ya mwaka 1928 ili kukidhi mahitaji.
Aidha, imewataka wananchi wasikubali kujihusisha na madalali ambao hawajasajiliwa, kwani wanafanya kazi hiyo kinyume cha sheria na wanainyima Serikali mapato.
Sheria hii inatambua kuwepo kwa shughuli za dalali kama mtu yeyote anayeuza mali inayohamishika au isiyohamishika. Sheria ya Madalali inampa mamlaka Katibu Mkuu Hazina kutoa leseni kwa madalali kupitia wilaya anayokaa mwombaji au anayotarajia kuweka shughuli zake za udalali," alisema Naibu Waziri
Hata hivyo, sheria yetu ya madalali haitoi mamlaka kwa madalali kufanya shughuli za upangishaji wa ardhi na majengo. Sheria haisimamii au kudhibiti mawakala wanaojishughulisha na uwakala wa majengo na ardhi. Pia ni kweli sheria yetu ya madalali ni ya muda mrefu, miaka 85," alisema Salum na kuongeza:
"Ni kweli wapo madalali ambao hawajasajiliwa na Hazina wanafanya kazi hiyo. "Tunawaomba wabunge na wananchi kwa ujumla tushirikiane kuwafichua watu hao. Kama nilivyoeleza, sheria ina mapungufu makubwa, hivyo kwa sasa tushirikiane kuwafichua wakati tukiandaa sheria mpya."
No comments:
Post a Comment