Sunday, 14 July 2013

MACHIMBO YA KOKOTO YAUWA WAWILI NA MMOJA KUJERUHIWA VIBAYA, WOTENI WA FAMILIA MOJA

JOSEPH WAMBURA NDUGU WA MAREHEMU NA MAJERUHI AKIWA AMELAZWA WODI LA WANAUME BAADA YA KUPOTEZA FAHAMU MUDA MFUPI TU BAADA YA KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUSHUHUDIA VIFO.

Julai 14,2013.
Serengeti:WATU wawili wakazi wa kitongoji cha Kanisani kijiji cha Matare Mamlaka ya mji wa Mugumu wilayani Serengeti wa familia moja  wamekufa na mmoja kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto.
Tukio hilo limethibitishwa na polisi,uongozi wa kitongoji na Hospitali teule ya Nyerere ddh limetokea julai 14 majira ya saa 4:10 asubuhi mwaka huu katika eneo la machimbo ya kokoto,wakati wakiwa wanachimba.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Juma Mahando amewataja waliofariki kuwa ni Rhobi Mwita Nyantori(45)ambaye alifia eneo la tukio,Nyahiri Chacha Mwita(41)ambaye amefariki baada ya kupata huduma na majeruhi ni Wegesa Mwita(39)ambaye amelazwa.
Akisimulia mkasa huo kwa kugugumia Wegesa ambaye ni majeruhi alisema wenzake walikuwa ndani ya shimo nay eye akiwa pembeni akisubiri mzigo wa kokoto aweze kutoa nje ghafla walianguliwa na kifusi chote na kuwafunika.
“Udongo wote umenifunika..kilichosaidia pembeni kulibaki kama uwazi,lakini waliokuwa ndani humo umewapiga wakiwa wameinama na kuanguka…watu waliokuwa nje waliona na kupiga kelele wakajitokeza watu wakatupa msaada…nahisi maumivu makali kiunoni na mbavu”alisema kwa kugugumia.
Mganga wa zamu dk,Amosi Kittoh amesema kilichopelekea kifo cha Rhobi ni kuumia kifuani na Nyahiri alipata madhara makubwa kwenye uti wa mgongo .
Dk ,Kittoh amesema kuwa tukio hilo limesababisha ndugu wa marehemu hao Joseph Wambura kupoteza fahamu na wamemlaza wodi ya wanaume kwa ajili ya matibabu.
Wegesa Mwita(39)mmoja wa majeruhi ambaye amelazwa,katika hospitali teule ya Nyerere ddh baada ya kuangukiwa na kifusi wakichimba kokoto,akisukumwa na mwenyekiti wa kitongoji cha kaniasani Matare wilayani Serengeti Juma Mahando.




 Wegesa Mwita(39)majeruhi katika tukio hilo.
 BAADHI YA NDUGU WAKILIA BAADA YA KUTAARIFIWA KUFARIKI KWA NYAHIRI CHACHA MWITA(41)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!