Saturday, 13 July 2013

JESHI LA POLISI LATEUA ASKARI WA KUMFUATA AGNESS MASOGANGE ALIYENASWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI


            
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti la ijumaa kwa simu jana kuwa watawapeleka polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjC3I-Xcn-7SlYUgYB1vWKcMW-om7c_TpCv4cZY886fgrCmutjMaNOnSgf9OtLxqSwuvb_RmkxyNf9BvLcUf6z8ODkiNGuYQUs3Rnh-94j89_E2yL4eLdjjYW2FGwZCrxPndUujpNIxuifX/s1600/MELISAEDWARD.jpg
   Mellisa Edward

Huyu ndie msichana aliyekuwa  na Agness Gerald. walipokamatwa na madawa ya kulevya huko Afrika ya kusini.  

    Jeshi la Polisi litapeleka askari wake Afrika Kusini kuwahoji washiriki wa video za wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa Edward waliokamatwa nchini humo na dawa za kulevya.



Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliiambia  Mwananchi  kwa simu jana kuwa watawapeleka polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo.


Wasichana hao walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine.


“Tutawapeleka askari wetu kuwahoji, tumekwishaanza uchunguzi wa hili...wote watakaohusika katika hili tutawakamata, lakini tunakwenda polepole hatua kwa hatua kuhakikisha tunawanasa wahusika sahihi,” alisema Nzowa.

Naye Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, (JNIA), Moses Malaki alieleza kushangazwa na kiasi kikubwa kupitishwa kwenye uwanja huo licha ya kuwa wapo watu wenye dhamana ya kuangalia usalama.


“Sitaki kusema tutafanya nini, lakini ninachotaka kukwambia ni kwamba uchunguzi umeanza na suala zima tumewaachia polisi na sisi tutatoa ushirikiano kwa kila hatua watakayotutaka, lazima kukomesha hili.


“Tutaangalia nani walikuwa zamu siku hiyo,” alisema Malaki



   


                             

 


 
 


 
 

 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!