Monday, 8 July 2013

HABARI ZA UMBEYA ......MITUSI YA NGUONI ATUKANWA IRENE UWOYA, KISA DIAMOND

Na Gladness Mallya MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya matusi baada ya kumfananisha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa mwanamuziki mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson.

Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuwa msanii huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye staa atakayemrithi mkali huyo wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi hayo ya nguoni.

Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa na kufananisha vitu ambavyo havina uwiano hasa ukizingatia Michael Jackson alishafariki dunia Juni 25, 2009.

“Sasa hiyo ni akili gani ya ki…(tusi) kumfananisha mtu aliyeko hai na marehemu?” alihoji Mishish, mmoja wa mashabiki wa Uwoya katika mtandao wa Facebook, "kweli wewe Irene ni......( tusi) au kwasababu Diamond amesha.....(tusi).

CHANZO GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!