Sunday, 9 June 2013

KATIBA MPYA ILIYOTANGAZWA INAHITAJI KUFANYIWA KAZI.............ASEMA SAMWELI SITA.




Waziri wa ushirikiano waAfrika Mashariki Mh. Samweli Sitta amesema mchakato wa rasimu ya katiba mpya iliyotangazwa imelenga kuwatafutia ulaji viongozi wa serikali na kwamba inahitajika kufanyiwa kazi ya ziada na kudai kuwa muungano au shirikisho haviwezi kupatikana kama vipengele vinavyohusu serikali ya tanzania bara havijaelezwa vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kwenye mahafali ya chuo cha Ualimu Kibamba Mh Sitta amesema endapo kutakuwepo na rais wa tanganyika ina maana nchi itakuwa kihoja kwa kuwa na marais watatu na kueleza kuwa kama yakipitishwa basi wananchi wakubali kuwepo na mzigo wa kuwahudumia na hata itifaki yake itakuwa ni tabu na kudai kuwa rasimu hiyo ni dhahiri viongozi wanajitafutia ulaji ndani ya katiba mpya kwani haelewi ni kwanini tume imependekeza mawaziri 15 wakati masuala ya muungano yapo saba

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!