Friday, 14 June 2013

WACHEZAJI WA IVORY COAST WAKUNJANA MASHATI KABLA YA MECHI NA TAIFA STARS.




Wachezaji wawili wa Ivory Coast wametimuliwa kwenye kikosi kinachojiandaa na mchezo kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya Tanzania unaotarajiwa kupigwa uwanja wa Taifa siku ya Jumapili.
 

Mchezaji wa zamani wa Monaco Jean-Jacques Gosso Gosso, 30, ambaye kwa sasa anacheza kwenye ligi ya Uturuki akiichezea Mersin na kinda la miaka 20 Abdul Razack wa Manchester City, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Charlton Athletic, walipigana siku ya jumatano wakati timu yao ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuelekea Tanzania .

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!