Monday, 24 June 2013

NGASSA ARUDISHWA SIMBA.

                                     
Khadija Mngwai na Joan Lema

SHAUKU ya mashabiki wa Yanga ya kumuona kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa akivaa tena uzi wa Jangwani huenda ikapotea baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutamka kwamba Ngassa ni mchezaji halali wa Simba.

Ngassa alitua Yanga hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Simba ambako alikuwa akicheza kwa mkopo kutoka Azam, lakini Simba ilidai ilimsainisha mkataba wa mwaka mmoja, uliopangwa kuanza kutumika msimu ujao, baada ya huu wa mkopo kuisha msimu uliopita.

TFF imesema inamtambua Ngassa kama mchezaji wa Simba kwa kuwa mkataba aliosaini na klabu hiyo upo katika Ofisi za shirikisho hilo na umesajiliwa, na pia imesema haiutambui mkataba wa Ngassa Yanga, kwa kuwa klabu hiyo imemsaini kinyemela, bila kuupeleka mkataba wake katika shirikisho hilo ili kusajiliwa kama ilivyo kawaida.




SOURCE GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!