skip to main |
skip to sidebar
HUYU NDIYE MWANAFUZI WA UDSM ALIYEPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI, HAYA NI MAELEZO KWA YALIYOTOKEA.
Mwanafunzi , Alex Robert wa mwaka wa nne na wa mwisho katika kitivo cha sheria pale mlimani jijini DSM.
Usiku wa kuamkia jana alipokua akijisomea na kuandaa "Disertation" na wenzake, walijikuta wakivamiwa na majambazi na kuamuliwa watoe "computer" zao na pochi za fedha.
Walikubali wakawapa computer na pochi na majambazi yakaanza safari yao.
... Kutokana na umuhimu wa kazi waliyokuwa wakiiandaa na uchungu wa elimu aliokuwa nao kijana Alex Robert aliamua kuwafuata majambazi walipokua wakiondoka ili angalau apate hata soft copy ili kazi yao isipotee, bahati mbaya haina mwenyewe, alipigwa risasi ya tumboni na yale majambazi bila huruma, yalimwacha akigalagala chini bila msaada.
Kwa sasa yupo katika hospitali ya taifa ya muhimbili akiwa amekwisha kufanyiwa oparesheni
No comments:
Post a Comment