Monday, 24 June 2013

HALI YA RAIS WA ZAMANI WA AFRICA YA KUSINI IMEKUWA SI NZURI KWA SAA 24 ZILIZOPITA

Madaktari wanaomtibu rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.
Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.
Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela jumapili jioni na kuzungumza na jopo la matatibu wanaomtibia.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!