SERIKALI imewaagiza watendaji na wananchi kupitia kamati za o za afya kuhakikisha misamaha inatolewa kwa wote wanaostahili.
Aidha imesema kuwa kituo ambacho hakifanyi vizuri katika ukusanyaji na udhibiti wa matumizi ya fedha zinazotokana kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), viongozi husika wapewe onyo. Baada ya muda watakaopewa iwapo hakuna mabadiliko zichukuliwe hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuondolewa madaraka waliyopewa.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi wakati akifungua mkutano wa mkutano mkuu wa mwaka wa waganga wakuu wa mikoa , wilaya na baadhi wa wakurungezi wa hospitali za rufaa na taasisi za wizara hiyo wakiwemo wakurugnezi wa asasi za kiraia, wadau wa maendeleo na washiriki kutoka Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI).
Mkutano huo wa siku tatu umefanyik katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment