Wednesday 22 May 2013

VURUGU MTWARA, ASKARI WANAOKADIRIWA WATANO WAPOTEZA MAISHA WAKIWA NJIANI KWENDA KUTULIZA GHASIA, MILIO YA MABOMU NA RISASI VYATAWALA.


Ofisi zachomwa moto
Ofisi zachomwa moto


Magari ya manispaa nayo yachomwa moto
Magari ya manispaa nayo yachomwa moto


Ambulance nayo yachomwa moto
Ambulance nayo yachomwa moto

Tunahabarishwa kuwa hali ni mbaya huko Mtwara. mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka n.k
Habari hizo zimeongeza kuwa  Daraja la Mikindani limevunjwa na hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam.
Kwa mujibu wa habari zisizo na uthibitisho, baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi 
 
Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
 
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam.
Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto. 
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.
 
Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika. 
Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani
 
 
Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi. 
 
 
 
 
 .
Habari kwa hisani ya mpekuzi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!