Thursday 23 May 2013

RASILIMALI YA NCHI NI MALI YA TAIFA ZIMA..................WALIOSABABISHA VURUGU MTWARA KUKIONA CHA MOTO!

 
 
 
 

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewaonya watu wanaosababisha uvunjifu wa amani nchini humo kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
Onyo hilo linafuatia ghasia ambapo ofisi kadha, maduka na nyumba zimechomwa katika mkoa wa Mtwara ulioko kusini mashariki mwa Tanzania jana
 

 Rais Kikwete amesema wale wote waliokamatwa na polisi wakati wa ghasia hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe ni fundisho kwa wengine wenye lengo la kuvuruga amani ya nchi. Raisi ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika Television ya Taifa ya TBC1 jijini Dar-es-salaam.
 
Ghasia hizo zilianza muda mfupi baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni. Akizungumzia madai ya waandamanaji hao, Rais Kikwete amesisitiza kuwa raslimali za nchi ni mali ya taifa zima.
 

Amesema mkoa wa Mtwara haujatelekezwa na kusema kwamba kuna mipango ya kutumia gesi hiyo kujenga viwanda vya mbolea na kutumia gesi hiyo asilia kuzalisha nishati ya umeme kwa mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma ili kuunganishwa katika gridi ya taifa
 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!