Friday, 10 May 2013

POLISI WATATU WAKAMATWA NA FUVU LA KICHWA CHA BINAADAMU, WAMEDAIWA KUTAKA KUMMBAMBIKIA KESI RAIA ASIE NA MAKOSA.







Jeshi la Polisi limeendelea kupata kashfa, baada ya askari wake watatu mkoani Morogoro na raia mmoja kushikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la kichwa cha binadamu ambalo walikuwa wanalitumia kubambikia watu kesi.


Askari hao wanaofanyakazi katika wilaya ya Kilosa wanadaiwa kujaribu kukitumia kichwa hicho kutaka kumbambikia kesi mfanyabiashara mmoja mkoani humo.

Fuvu hilo linadaiwa ni la mtu aliyeuawa hivi karibuni kati ya wilaya za Kilosa na Mvomero mkoani humo.

Tukio hilo limevuta hisia za watu wengi ambao walikusanyika katika kituo cha polisi katika mji wa Dumila ambako watuhumiwa hao wanashikiliwa.

Mmoja wa wananchi hao, Saleh Omar, mkazi wa Dumila, aliwatuhumu askari hao kushirikiana na raia mmoja kumbambikia kesi hiyo mfanyabiashara ya maduka katika mji wa Dumila, Samson Mura.


Alisema Jumatatu wiki hii, walifika askari watatu na raia mmoja ambaye naye alijitambulisha ni askari wakiwa na mfuko usiojulikana ndani yake kuna nini na kwenda nyumbani kwa mfanyabiashara huyo wakitaka kumfanyia upekuzi nyumbani kwake kwa madai kuna vitu vya wizi amevihifadhi

 Hata hivyo, Mura aliwaruhusu askari hao watatu na raia huyo aliyejitambulisha kuwa ni askari kuingia katika nyumba hiyo na kuanza upekuzi, lakini hawakufanikiwa kupata kitu chochote.

Baadaye askari hao walimtaka mfanyabishara kutoka nje na kufungua gari lake ndogo milango ya mbele, lakini nako hawakukuta kitu na baadaye mlango wa nyuma na ndipo walipokiweka kichwa hicho kwa siri na kumtuhumu kuwa alikuwa amefanya mauaji



Habari kwa hisani ya Mpekuzi..



1 comment:

msema kweli said...

Hiyo ndio Bongo bwana, sasa hao ndio polisi wa kibongo walivyo

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!