Thursday 23 May 2013

MAJAMBAZI YAVAMIA GARI NA KUPORA MAMILIONI YA FEDHA, JIJINI DAR-ES-SALAAM LEO ASUBUHI.

Hayo ni matundu ya risasi yaliyopigwa na majambazi kwenye kioo cha dereva na kwamaba , majambazi hayo kufanikiwa kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 na kutokomea nazo.
 Kutokana na watu walioshuhudia ujambazi huo,wanasema tukio hilo  lililofanyika maeneo ya Sayansi mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano Asubuhi.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda piki piki,ghafla wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili wa namba T929 CCX  kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine gun na wengine walikuwa na bastola.
 Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi.



Habari kwa hisani ya mpekuzi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!